Ticker

6/recent/ticker-posts

FAINALI ZA MAVUNDE CUP KATA YA IPALA ZAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA


***************

Fainali za Kombe la Mavunde zimehitimishwa jana huku Timu ya Chipukizi FC ya Mahomanyika wakiibuka mabingwa kwa kuifunga Timu ya Ipala FC kwa mikwaju ya penati 3-1.

Mgeni Rasmi wa fainali hizo alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ambaye ameahidi kuboresha zaidi mashindano hayo ili kuibua na kuendeleza vipaji Jijini Dodoma.

Katika mashindano hayo Mbunge Mavunde amegharamia vifaa vya michezo kwa Timu zote kumi na zawadi za washindi ambapo jumla yake ni kiasi cha Tsh 3,500,000

Wakishukuru kwa niaba ya wanamichezo wote,Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuchochea maendeleo ya michezo katika Kata ya Ipala na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega kukuza vipaji vya vijana katika eneo hilo

Post a Comment

0 Comments