Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda, akizungumza na wadau wa maendeleo wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo ya jamii na maafisa wa mfuko wa jamii Tasaf
Mkurugenzi wa program za jamii wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), John Elisha akiangalia bidhaa zilozotengenezwa kwa mikono na wanufaika wa mfuko wa tasaf wakati walipofanya ziara na wadau wa maendeleo kutoka ubalozi wa Sweden na Ireland. Wengine pichani ni wadau wa maendeleo kutoka Balozi la Sweden na Ireland.
Mkurugenzi wa program za jamii wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), John Elisha akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda (katikati), pamoja na Meneja wa program ya maendeleo jumuishi ya kiuchumi kutoka ubalozi wa Sweden Annie Sturinge (kulia), wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na maafisa wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF),
Meneja Uchumi shirikishi kutoka ubalozi wa Ireland Eric Masinda akiuliza swali wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo ya jamii na maafisa wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kwaajili ya kujifunza Mambo mbalimbali.
..............................................
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda amesema miradi ya TASAF na juhudi za halmashauri kuwawezesha wananchi zimepunguza kwa kiwango kikubwa hali ya umasikini Wilayani Bagamoyo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Shauri Seleda ameyasema hayo leo wakati Maofisa wa TASAF na ubalozi wa Sweden walipotembelea katika halmashauri hiyo ili kujionea miradi inayotekelezwa na walengwa kutoka Kaya Masikini wilayani humo.
Amesema kwa sehemu kubwa wanaopewa mikopo na Halmashauri ni wale ambao tayari wamenufaika na miradi mbalimbali ya TASAF na wanajua namna ya kuendesha ujasiriamali mbalimbali.
"Tunawapa mafunzo kwanza na hilo limesaidia sana maana wengi tunaowapata ni wanawake na kwa kawaida Pwani hawa ndiyo wanaotunza familia," amesema Selenda.
Mmoja wa wanufaika wa TASAF Zena Hassan amesema uwezeshaji alioupata kutoka TASAF umemuwezesha kusomesha watoto wake wanne na kujenga nyumba yenye thamani ya Shilingi milioni 8 katika kipindi cha miaka mitatu.
"Kwa namna ambavyo nimenufaika na kujengwa kiujasiriamali sasa naweza kusimama mwenyewe hata utakapofikia muda wa kuondolewa kwenye orodha ya wanufaika," Amesema Zena
Naye Mkurugenzi wa Program za jamii za TASAF John Elisha amesema TASAF hivi sasa inatekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wananchi kiujasiriamali ili kuwaondoa katika umasikini, mradi huo wa mabilioni ya Shilingi ulianza mwaka 2020.
Meneja wa programu ya maendeleo jumuishi ya kiuchumi kutoka ubalozi wa Sweden Annie Sturinge amesema maendeleo ya watu ni jambo muhimu kwa taifa lolote lile "Maeneo mengi tunayoenda huwa tunatamani kuona wanufaika wa TASAF wanachangamkia fursa nyingine za mikopo na hilo limefanyika Bagamoyo"
0 Comments