Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY-- BORESHENI HUDUMA ZA TIBA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na watumishi wa Idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza na Idara mbalimbali Kwenye wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akiongea na watumishi wa Idara ya tiba
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifello Sichalwe akiongea Jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Waziri Ummy Mwalimu Akizungumzia na watumishi.

************************

Na. WA-Dodoma

Hospitali za rufaa za mikoa nchini zimetakiwa kuboresha huduma za afya pamoja na kuwa na mawazo mapana katika kuboreshaji wa miundombinu ya hospitali hizo ili kuweza kuisaidia na kuipunguzia mzigo hospitali ya Taifa ya Muhimbili,

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wafanyakazi wa idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na kufanya mapitio ya idara mbalimbali zilizopo kwenye wizara hiyo

Mhe. Ummy amesema ili kuonesha kweli idara ya tiba ndio inayobeba wizara hiyo hamna budi kuboresha huduma hizo ili zilingane na mahitaji ya wananchi kwani wananchi wanaziamini hospitali za umma.

“tunatakiwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya ni mzuri, hivyo ni wakati wa kuangalia changamoto na kuziboresha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wanafika kwenye vituo vyetu kupata huduma“ amesema Mhe. Ummy.

Aidha, Waziri huyo ameitaka idara hiyo kufanya upya mapitio ya miongozo ya utoaji huduma ili kufanya huduma zinazotolewa kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa zinakuwa bora na zenye manufaa kwa wananchi vilevile miongozo hiyo iweze kuunganisha vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hata hivyo Waziri Ummy amewataka watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kama timu na endapo kuna changamoto ni vyema zikajadiliwa kwa pamoja ili kwenda kwa pamoja katika kuboresha huduma za afya nchini.

Post a Comment

0 Comments