Ticker

6/recent/ticker-posts

WASHINDI 100 WA NMB MASTABATA WAZAWADIWA 10M



***********************************

Na Mwandishi Wetu

Wateja 100 wa kwanza wa kampeni ya NMB MastaBata-Kivyako Vyako walipatikana jana nakuzawadiwa pesa taslimu TZS 100,000 kila mmoja nataasisi hiyo kiongozi wa shughuli za kifedha nchini.
Washindi hao wamezawadiwa jumla ya TZS milioni 10.

Promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako ilizinduliwarasmi katikati ya mwezi Disemba mwaka jana kwa lengola kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za Mastercardkama sehemu ya mchango wa NMB katika juhudi zataifa za kujenga uchumi usiotegemea sana fedhataslimu.

NMB pia inatumia kampeni hii ya kuendeleza uchumi wakidijitali kurudisha fadhila kwa wateja wake waaminifuambao wamekuwa ni muhili muhimu wa safari yake yamabadiliko ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata washindi wakwanza wa MastaBata-Kivyako Vyako, MenejaMwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ali Ngingite, alisema zaidi ya TZS milioni 200 zitanyakuliwakwenye kampeni hii ya miezi mitatu.

“Hili ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanzarasmi mwaka 2018 kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za Mastercardwanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti,” mtaalumu huyo wa mikopo binafsi alisema.

“Kama watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo la kuwatambua nakuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendeleakutumia huduma zetu,” Bw Ngingite aliongeza nakutabainisha kuwa zitakuwepo pia droo za kila mwezi naile kubwa ya mwisho.

Wakati washindi 100 wa kila wiki watashinda TZS 100,000 kila mmoja, 25 watanyakua TZS 1,000,000 kilamwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya TZS milioni 90 zikiwa ni TZS milioni kwa kila mshindi.

Bw Ngingite alisema takribani wateja 1,000 wanategemewa kushinda zawadi za promosheni yaMastaBata-Kivyako Vyako iliyopangwa kufikia tamatimwezi Machi.

Kampeni hii inawahusisha pia wateja wa benki hiyowanaofanya malipo kwa NMB MasterPass QR. Kama kawaida droo ya jana ilisimamiwa na ofisa mwandamiziwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

NMB inasema kampeni zake za MastaBatazimefanikiwa sana kuchagiza malipo ya kidijitali nchinina matumizi ya kadi za Mastercard kufanya malipo namiamala mbali mbali.

Mwezi Novemba mwaka jana, kampuni ya MastercardInternational iliitunuku NMB tuzo maalumu ya kuwabengi kiongozi wa kuhamasisha matumizi ya kadi zakenchini.

Post a Comment

0 Comments