Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MULEBA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAONDOLEA TATIZO LA UHABA WA MADARASA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Elias Mahwago aki tembelea shule ya Sekondari Kaigara iliyopo Kata ya Muleba wakati shule zilipofunguliwa leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Elias Mahwago akiangalia namna wanafunzi wanasoma wakati wa ziara yake ya kutembelea shule ya Anna Tibaijuka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muleba Ndg. Elias Mahwago akiangalia namna wanafunzi wanasoma wakati wa ziara yake ya kutembelea shule ya Anna Tibaijuka


*********************************

NA MWANDISHI WETU,KAGERA.


WANAFUNZI wanaosoma kwenye Shule zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wameondokana na changamoto za uhaba wa madarasa baada ya kuanza shule leo wote wakiripoti shuleni na kusomea kwenye madarasa yaliyojengwa kwa Fedha kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Mkopo wa IMF.


Akizungumza mara baada ya kutembelea shule ya Sekondari Kaigara iliyopo Kata ya Muleba wilayani Muleba Mkoani humo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Elias Mahwago Kayandabila alisema wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa madarasa mapya ambayo yamesaidia kuondoa uhaba ambao ungeweza kujitokeza kwa sababu Wilaya hii ya Muleba intarajia kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza 13,360 na sasa wote watakaa katika Madarasa Ya Samia, kwa hakika HISTORIA IMEANDIKWA alisisitiza Mkurugenzi Kayandabila.


Alisema kwamba Halmashauri ya Muleba walipokea wilaya nzima Bilioni 4.680 kutoka Serikali kuu ambapo wamejenga madarsa 234 hivyo kuondoa kabisa changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati.


Ambapo kwenye picha zipo Shule za Sekondari Kaigara na Shule za Sekondari Anna Tibaijuka kutoka Muleba na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza walioanza leo kutumia Madarasa Ya Samia.


“Kwa kweli tuna kila sababu ya kujivunia kuwa na Rais Samia Suluhu kwani tumepata fedha nyingi Muleba ili watoto wetu wasome hivyo kutokana na mazingira mazuri kama hayo leo tumewapokea watoto takribani 72 na wamekwisha kusajiliwa na wengine wanaendelea kusajiliwa hapa Shule ya Sekondari Kaigara, alisema Mkurugenzi Kayandabila.


Hata hivyo alisema leo hii aliweza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya shule za Sekondari ili kuona namna ya wanafunzi wanavyopokelewa bila changamoto ya aina yoyote ile.


Awali akizungumza Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Shule ya Sekondari Anna Tibaijuka Ester Meshaki alisema wanashukuru Rais Samia Suluhu kwa kuto fedha hizo za kuwajengea madasa ya kisasa nao wanamuhaidi kusoma kwa bidhii ili nao waweze kufika ndoto zao.


Naye mwanafunzi mwengine wa Shule hiyo alisema kwamba kipeke wanamshukuru Rais Samia kwa kuwajengea madrasa mzuri na wanamuhaidi watasoima kwa bidhii ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.


Hata hivyo Mzazi kutoka Kijiji cha Mahalahala kutoka Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera ambaye alimpeleka mtoto wake shuleni alisema wanashukuru kuona Madarasa ya Samia yamekamilika huku wakitoa pongezi zao kwa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu.


Alisema pia wanamshukuru Rais Samia kwa kuwaepusha na michango waliokuwa wakichngishwa na wanamuombea kwa Mungu amtangulie kwenye kazi zake .

Post a Comment

0 Comments