Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI ZAIDI YA 250 MGODI WA MPIPITI SINGIDA WATIMKIA CCM

Vijana wa Skauti Idd Jumanne (kulia) na Salum Hassan wakimvika Skafu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida William Nyalandu baada ya kuwasili Shule ya Sekondari ya Mudida iliyopo Kata ya Mudida wilayani Singida wakati akizindua maadhimisho ya miaka ya 45 tangu kuzaliwa CCM yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida William Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Mudida wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida William Nyalandu akipanda mti katika viwanja vya shule hiyo wakati wa maadhimisho hayo. Kulia ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Singida Zainabu Abdallah na katikati ni Mkuu wa Shule hiyo, Khalid Mambuli.
Wanafunzi wa shule hiyo wakifanya gwaride maalumu kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Mkuu wa shule hiyo Khalid Mambuli akitoa taarifa ya shule hiyo ya ujenzi wa madarasa yaliyo jengwa kwa fedha za mradiwa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 ambapo walipokea Sh.60,000 Milioni.
Walimu wa shule hiyo wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Singida, Athony Katani akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Singida Zainabu Abdallah akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Naomi Daudi akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Singida Ezekiel Lissu akizungumza.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mudida wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Ilongero Stellah Nghwasi akimtoa damu Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Singida Ezekiel Lissu wakati wa zoezi la kuchangia damu kwa hiyari.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa tayari kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni moja ya kazi iliyofanyika kwenye maadhimisho hayo.
Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Ilongero Stellah Nghwasi akimtoa damu mwanafunzi wa Kidato cha pili wa shule hiyo Anthony Edward kwa ajili ya kusaidia akiba ya damu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu (kulia) akiongoza kufanya usafi katika eneo la Mgodi wa Mpipiti ikiwa ni kazi mojawapo ya maadhimisho hayo. Katikati mwenye suti ni mmoja wa Mameneja wa mgodi huo Hamisi Gunda.
Kazi ya kufanya usafi ikiendelea.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida Neema Sambaa (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Singida Ezekiel Lissu wakipanda mti eneo la Mgodi wa Mpipiti.
Zoezi la kupanda miti likiendelea.
Wakina mama wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wachimbaji wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Mmoja wa wakurugenzi wa mgodi huo Mussa Maduhu akihamasisha uchangiaji kwenye harambee ya kupata fedha ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM wilayani humo.

Mchimbaji Onesmo Mwanga akisalimiana na viongozi waliopo meza kuu.

Katibu wa mgodi huo, Juma Isango akisoma risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu wa CCM Kata ya Mudida Juma Kitiku akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mudida Salehe Satu akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Wakurugenzi watatu wa mgodi huo wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kulia ni Rachel Bunangu, Hamisi Gunda na Mussa Maduhu.
Wazee wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wakina mama wazee wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wanawake Wajasiriamali kwenye mgodi huo wakiwa katika maadhimisho hayo.
Wachimbaji wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Kituo cha Polisi katika machimbo hayo Mkaguzi wa Polisi, Isaya Mwidete akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Singida Alex Mbogho akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida Neema Sambaa akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Singida Hamisi Nkungu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.


Mchimbaji Aldofu Saida akipongezwa na viongozi meza kuu baada ya kuhamia CCM.
Mchimbaji Aldofu Saida akionesha kadi ya CCM baada ya kuhamia chama hicho akitokea Chadema.
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Mudida, Joseph Muri akimpongeza Aldofu Saida baada ya kuhamia CCM.
Mjasiriamali Jackline Daniel akisalimiana na viongozi meza kuu baada ya kujiunga CCM.
Wajasiriamali katika mgodi huo wakiserebuka baada ya kujiunga na CCM.
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utii baada ya kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Anthony Katani (kushoto) akiwaongoza kula kiapo wanachapa wapya waliojiunga CCM.
Maadhimisho yakifanyika.
Mkurugenzi wa mgodi huo Mussa Maduhu akichangia katika harambee wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Singida.
Wajasiriamali katika mgodi huo wakiserebuka na kufurahi baada ya kujiunga CCM
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu (kulia) akitoa zawadi ya madaftari kwa wanafunzi wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu (kulia) akitoa zawadi ya sabuni kwa wazee.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya CCM wilayani humo baada ya kufanya harambee ya papo kwa papo kwa ajili ya kumsaidi Samwel Mdimi kutengeneza baiskeli yake ambapo zilipatikana Sh.100,000. Kulia ni Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Haruna Ntandu ambaye alisema Mbunge wa jimbo hilo Ramadhani Ighondo amefanikisha kupeleka umeme kwenye machimbo hayo.






****************

Na Dotto Mwaibale, Singida




WAFANYAKAZI zaidi ya 250 wa Mgodi wa Mpipiti uliopo Kata ya Mudida wilayani Singida mkoani hapa akiwemo aliyekuwa mgombe udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Maswa mkoani Simiyu, Aldofu Saida wameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Nyalandu aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani humo walisema wameamua kujiunga na chama hicho baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye wamemuomba awakumbuke kuwajengea miundombinu hasa daraja la mto Mpipiti ambalo ni la muhimu sana kwao kulitumia kwenda kwenye mgodi huo.

Walisema kutokuwepo kwa daraja hilo kumekuwa na changamo kubwa ya kufika katika mgodi hasa kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha ambapo watumiaji wa eneo hilo hasa wachimbaji wa madini na wananchi wanaoishi jirani na mgodi kuhatarisha maisha yao kwa kusombwa na maji vikiwemo vyombo vya moto kama pikipiki na magari yanayopita eneo hilo kwa hofu ya kusombwa na mafuriko.

Mmoja wa Wakurugenzi wa mgodi huo Mussa Maduhu alisema changamoto kubwa waliyonayo ni kujengewa daraja hilo, kukatika kwa umeme mara kwa mara ambapo unakwamisha utoaji wa maji mengi maduarani na gharama kubwa ya kupeleka miti ya kufungia maduara kwa ajiri ya usalama wa kazi.

Alisema mgodi huo unakadiriwa kuwa ni wa pili kwa uzalishaji kimkoa baada ya mgodi wa Sekenke ulioko wilayani Iramba.

Maduhu alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania John Bina na uongozi wa ofisi ya madini Mkoa wa Singida kwa ushirikiano mkubwa wanaowapa katika masuala yote ya uchimbaji.

"Tumekuwa na changamoto nyingi lakini utatuzi wake umekuwa ukichukua muda mrefu baada ya kuwepo kwa ahadi nyingi hewa tunazoahidiwa na baadhi ya viongozi waliowahi kufika hapa mgodini kujua changamoto zetu" alisema Maduhu.

Aidha Maduhu aliwashukuru wachimbaji wote nchi nzima kwa kufanya kazi kwa bidii katika mazingira ya amani na utulivu na kuwa hali hiyo ndiyo imekuwa ikichangia kupata madini mengi na kuingizia Serikali mapato mengi pamoja na wao kuinuka kiuchumi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Nyalandu aliwaomba wanachama wa chama hicho utakapo wadia muda wa kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa chama hicho mapema mwezi ujao wachague viongozi wenye weledi ili waweze kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Nyalandu aliwataka Wana CCM kukihimarisha chama kwa kushirikiana na kulipia ada za uanachama kupitia mfumo wa kielektroniki na akawahimiza wanaohusika na mgodi huo kuzingatia usafi wa mazingira kama wanavyoelekezwa na viongozi wao.

Aidha akikagua madarasa ya Shule ya Sekondari Mudida yaliyo jengwa kwa fedha za mradiwa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kumuheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan aliyetoa fedha hizo kwa nchi nzima na wazazi kwa uongeza ufaulu na kujiepusha na vitendo vitakavyo wasababishia waache shule au kupata mimba wakiwa shuleni kwani wao ndio wanaotegemewa kuwa viongozi wa kada mbalimbali hapa nchini.

"Kwa kuwa mmepata madarasa mazuri ya kusomea someni msidanganyike na vizawadi kama chipsi, fedha na waendesha bodaboda ambao wanaweza kuwakwamisha mshindwe kuendelea na masomo yenu" alisema Nyalandu.

Katibu wa UVCCM wa Wilaya ya Singida Zainabu Abdallah alisema katika maadhimisho hayo shughuli walizozifanya ni kufanya usafi wa mazingira katika Mgodi wa Mpipiti, kupanda miti,uchangiaji damu ambapo walipata uniti 50 na kutoa msaada wa sabuni na madaftari kwa watu na wanafunzi kutoka makundi maalumu.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo William Nyalandu aliendesha harambe ya kupata fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya nyumba ya Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo iliyoandandaliwa umoja huo chini ya katibu wake Zainabu Abdallah ambapo zaidi ya Sh. 1 milioni zilipatikana huku Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Anthony Katani akiendesha harambee ya papo kwa papo kumchangia Samwel Mdimi ambaye ni mlemavu apate Sh. 60,000 ili aweze kutengeneza baiskeli yake ya magurudumu matatu ambapo zilipatikana Sh.100,000 baada ya Mkurugenzi wa mgodi huo Mussa Maduhu kuongeza Sh.40,000 ambazo alikabidhiwa zimsaidie kwa mahitaji mengine na chakula huku mkurugenzi huyo akiahidi kuitengeneza.

Post a Comment

0 Comments