Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WA MAJI BONDE LA KATI WAKUTANA SINGIDA KUJADILI MPANGO WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI BONDE LA KATI

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Dk. George Lugomela (Wa pili kushoto) kwa niaba ya Katibu Mkuu akikata utepe kuashiria kuzindua Tafsiri Rahisi ya Mpango Jumuishi wa Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji Bonde la Kati wakati akizindua Jukwaa la Pili la Wadau wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati mjini hapa jana. kutoka kulia ni Katibu Muhutasi Bodi ya Maji Bonde la Kati, Happiness Mlingi, Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi za Bonde la Kati, Nelea Bundala na Kaimu Afisa Maji Bonde la Kati, Danford Samson.
Afisa Maji Bonde la Kati Danford Samson. akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kutoka kulia ni
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida katika kikao hicho Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Mang'alu Butondo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati Msaru Msengi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Samson Babala, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati Msaru Msengi.akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Kaimu Mkurugenzi Rasilimali za Maji na Mwenyekiti wa Mabonde yote Tanzania na Afisa wa Maji Bonde la Pangani, Segule Segule akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Wataalamu kutoka Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Kati wakifuatilia uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida katika kikao hicho Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Mang'alu Butondo akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara, Alistides Kakulu akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Singida katika uzinduzi huo Ally Mwendo akichangia jambo.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Beatus Choaji akizungungumza kwa niaba ya Katibu Tawala kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Juma Kilimba akichangia jambo.
Wadau wa maji wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto wakiokaa ni Kaimu Afisa Maji Bonde la Kati Danford Samson, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati Msaru Msengi na Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida katika uzinduzi huo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Mang'alu Butondo.
Wadau wa Maji wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Uzinduzi ukiendelea.
Mapitio ya Tafsiri Rahisi ya Mpango Jumuishi wa Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji Bonde la Kati yakifanyika baada ya kuzinduliwa.

************************

Na Godwin Myovela, Singida.


JUKWAA la pili la wadau wa maji Bonde la Kati limekutana mkoani hapa kujadili mambo kadhaa ikiwemo namna bora ya kukabiliana na changamoto za kupungua kwa vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi na namna bora ya kukabiliana na hali hiyo kwa ustawi na mustakabali wa watu na wanyama waishio ndani ya bonde hilo ambalo ni la pili kwa ukubwa likitanguliwa na Bonde la Rufiji.

Wadau hao kutoka kundi la watumia maji binafsi, Jumuiya za watumia maji, Halmashauri za Wilaya, Mamlaka za Maji, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, Sekta zinazohusiana na maji, Wizara ya Maji na Bodi za Maji za Mabonde, pamoja na mambo mengine, walipata fursa ya kupendekeza majina ya Wajumbe wa Bodi ya Sita ya Maji ya Bonde la Kati baada ya iliyokuwa bodi ya Tano kumaliza muda wake.

Pia kupitia kikao hicho wadau hao wa rasilimali za maji kwa pamoja walipitia mpango mkakati waliojipangia kuutekeleza katika Jukwaa la kwanza sambamba na kuandaa na mpango mkakati mwingine utakaotekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa.

Akizungumza jana wakati akizindua Jukwaa la Pili la Wadau wa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Dk. George Lugomela, kwa niaba ya Katibu Mkuu, alisema sheria, kanuni na miongozo mbalimbali imeandaliwa na ipo kisheria huku mingine ikiwa mbioni kukamilika lengo hasa ni kuendelea kuelekeza kwa kina jinsi ushiriki wa wadau wa sekta mtambuka unavyotakiwa kuzingatiwa katika ulinzi, uhifadhi, utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Lugomela katika mkutano huo uliobebwa na kauli mbiu ‘Vyanzo vya Maji, Uhai Wetu, Tuvitunze’ alisisitiza kwa kuwasihi wadau wa majukwaa hayo kushiriki kikamilifu katika kutekeleza shghuli zilizoainishwa kwenye mpango wa usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji bonde kwa tija inayolenga kuleta ustawi na uendelelevu wa rasilimali hiyo muhimu.

“Sasa tunapaswa kujikita zaidi kwenye kuyatambua mabonde madogo (vidaka maji) kwa maana ya kuzindua majukwaa mengi zaidi kwenye ngazi hii sambamba na kuyawekea utaratibu mzuri wa kisheria ili kuwezesha usimamizi thabiti wa mpango jumuishi uliopo wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji Bodi ya Maji Bonde la Kati,” alisema Lugomela

Hata hivyo Katibu Mkuu aliitaka ofisi ya bodi ya maji ya bonde hilo na mabonde mengine nchini kuanza kuangalia uwezekano wa kupanga na kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha majukwaa yote kuanzia ngazi ya taifa mpaka chini yanaanza kujiendesha chini ya uratibu wa kitaalamu wa wizara.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wadau wa bonde hilo Msaru Msengi alisema kwa sasa bodi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi hivyo kila mdau anawajibika kushiriki ipasavyo katika uhifadhi wa vyanzo vilivyopo.

“Kulingana na athari za mabadiliko ya tabia nchi vina vingi vya maji huenda vikaendelea kukauka au kupungua sasa ni jukumu la kila mmoja wetu kujikita katika kukabiliana na changamoto hizo ambazo zinaweza kuathiri watu wetu na wanyama tulionao ambao idadi yake ni kubwa ndani ya bonde hili,” alisema.

Awali, Kaimu Afisa wa Maji Bonde la Kati, Danford Samson pamoja na mambo mengine, alisema bodi hiyo mpaka sasa kwa kushirikiana na wadau imefanikiwa kuitisha jukwaa hilo kwa lengola kuweka mikakati na mpango kazi wa kushughulikia matatizo na changamoto zilizopo, kuandaa na kutekeleza Mpango Mkakati wa Bodi wa miaka 5, pamoja na kuandaa na kutekeleza mpango wa usimamizi wa pamoja na uendelezaji wa rasilimali za maji wa miaka 20.

“Kwa sasa tunaendelea na mchakato wa kuandaa mpango wa uhifadhi wa vyanzo vya maji (catchment conservation plan) na kutekeleza majukumu mengine ya kisheria ya bodi ya maji unaofanywa kupitia Sera ya Maji ya mwaka 2002 pamoja na Sheria ya usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009,” alisema Kaimu huyo Afisa wa Maji Bonde la Kati.

Post a Comment

0 Comments