Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akichangia jambo kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Mkutano ukiendelea Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliokuwa ukiendelea
********************
Tanzania imeungana na Nchi nyingine Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali uliofanyika leo tarehe 25/01/2022 kwa njia Video.
Mkutano huu umejadili kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria sambamba na kufanya tadhimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo na itifaki mbalimbali za Jumuiya.
Miongoni mwa Agenda zilizojadiliwa katika Mkutano huu ni pamoja na; majadiliano ya Ushauri wa Kisheria kuhusu Kufanya Mikutano ya Double Troika, majadiliano ya Ushauri wa kisheria kuhusu Mapitio ya Hadidu za Rejea za Kamati ya Mabalozi na Makamishna Wakuu wa SADC walioidhinishwa na Jumuiya hiyo, kupitia na kufanya Marekebisho ya Mkataba wa Mahakama ya Utawala ya SADC, kujadili Rasimu ya Mkataba wa Marekebisho ya Itifaki ya Maendeleo ya Utalii katika SADC na kujadili Mkataba wa Makubaliano ya Nchi Wanachama wa SADC kuhusu uanzishwaji wa Kituo cha Operesheni za Kibinadamu na Dharura cha Jumuiya.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi.
0 Comments