Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akifungua mafunzo ya Utekelezaji wa Kalenda ya mitaala yaliyofunguliwa mkoani hapa jana.
Mdhibiti Mkuu wa Shule Ubora wa Shule Kanda ya Kati Sostenes Magina akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Frederick Ndahani akitoa mada.
Afisa Taaluma Mkoa wa Singida Ayubu Mchana akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
********************
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKOA wa Singida umeenza kutoa mafunzo kwa maafisa elimu wa halmshauri, wathibiti ubora wa shule,maafisa wa TSC,maafisa elimu kata,wakuu wa shule na walimu wakuu katika Halmshauri ya Ikungi.
Akizingumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmshauri ya Ikungi amewataka Viongozi wa Elimu Kwa ngazi zote katika halmshauri yake kutumia kalenda ya Utekelezaji wa Mtaala ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika shule za awali, msingi na sekondari.
Kijazi alisema kalenda hii itakuwa nguzo na nyezo ya upimaji wa viongozi wa elimu kwa ngazi zote na walimu ili kubaini uwajibikaji wa viongozi hao.
Alisema kuwa kalenda hii pia itaondoa utofauti wa ufundishaji wa mada katika ya shule na shule,wilaya moja na nyingine pamoja na mkoa ,hivyo wanafunzi watapata mapata maarifa,ujuzi na stadi Kwa muda na wakati uliopangwa.
Akifafanua malengo ya Kalenda ya Utekelezaji wa Mtaala Mthibiti Mkuu wa Shule Kanda ya Kati Sostenes Magina alisema mtaala huu utatumika katika ukaguzi maendeleo ya Taaluma, ufundishaji na ujifunzaji shuleni ,amewataka walimu kuhakikisha klalenda hii inafutuatwa kikamilifu.
Afisa Elimu Taaluma Ayubu Mchana amewaeleza kuwa mtaala huu utasaidia mamalaka ya upimaji wa mtaala kuandaa mtihani kulingana na mada au maudhui yaliyofundishwa .
Mwezeshaji Frederick Ndahani amesisitiza walimu kuhakisha michezo inapewa kipaumbele kulingana na ratiba za shule,wamewataka wakuu wa shule na walimu wakuu kuhakikisha viwanja vyote vya michezo vinakuwa vusafi ndani ya wiki moja na kutumia ruzuku katika kipengele cha michezo kununua vifaa vya michezo, alisema kuwa michezo ni sehemu ya makuzi ya mtoto kiakili na kimwili.
Kwa upande wao walimu wakuu na wakuu wa shule wameipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu kuundaa Kalenda ya Utekelezaji wa mtaala nchini utakao wasaidia kusimamia kutekelezwa kwa kipindi kilichopangwa na kuondoa utofauti katika ya shule moja na shule nyingine.
Mafunzo yataendelea kufanyika kila Halmshauri ndani ya Mkoa wa Singida.
0 Comments