Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA MBEYA CITY


****************************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU yya Simba Sc imepoteza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi mara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya.

Mbeya City ilifanikiwa kupata bao lao la pekee kupitia kwa mshambuliaji wao Paul Nonga ambaye alipachika bao hilo dakika 20 ya mchezo katika kipindi cha kwanza mara baada ya kuwazidi nguvu mabeki wa Simba Sc na kuweza kupachika bao.

Mbeya City ilicheza pungufu toka kipindi cha kwanza mara baada ya nahodha wao kupata kadi mbili za njano na kuwafanya Mbeya City kucheza wakiwa pungufu uwanjani.

Licha ya kucheza pungufu Mbeya City ilionekana kuwa vizuri kuzuia ambapo kipa wao Dida Munishi alionekana shujaa kwa kuokoa michomo kibao kutoka kwa washambuliaji wa Simba Sc.

Simba Sc ilipata penati dakika 49 ya mchezo ambayo ilienda kupigwa na Chri Mugalu ambaye alifanikiwa kugonga mwamba na kushindwa kuingia kambani.

Post a Comment

0 Comments