Ticker

6/recent/ticker-posts

RC SINGIDA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA CHAKULA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Mahenge akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Muhalala katika ziara yake ya siku moja ya kukagua ugawaji wa mbegu za alizeti zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuwakopesha wananchi wilayani Manyoni mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mtaa Mkoa wa Singida Evodius Katale,
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mtaa Mkoa wa Singida Evodius Katale, akizungumza kwenye ziara hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Beatus Choaji akizungumzia kilimo cha alizeti katika ziara hiyo.
Afisa Kilimo Wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala akitoa taarifa ya kilimo cha zao la alizeti.
Mkururgenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeki akizungumza kwenye ziara hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama wakiwa kwenye ziara hiyo.
Mkutano na mkuu wa mkoa ukiendelea.
Katibu Tawala Wilaya ya Manyoni, Charles Mkama akizungumza.
Diwani wa Kata ya Muhalala David George akizungumza.
Mkutano ukiendelea.
Mkulima Francis Emanuel akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Jumanne Mlagaza akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa Kilimo Kata ya Muhalala, Christina Fanuel akitoa taarifa ya ugawaji mbegu mbele ya mkuu wa mkoa.
Mkulima Anderson Mlimo akiuliza swali.
Mkulima Yona Chitanda akiishukuru Serikali kwa kuwapelekea mbegu za alizeti.


******************

Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge amewataka wananchi mkoani hapa kutunza chakula walichovuna msimu uliopita ili kujihami kutokana na upungufu wa mvua ambao upo maeneo mengi nchini.

Dk.Mahenge aliyasema hayo katika ziara yake ya siku moja aliyoifanya Kijiji cha Mhalala wilayani Manyoni wakati akikagua ugawaji wa mbegu za alizeti zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuwakopesha wananchi.

"Msitumie hovyo chakula mlichovuna msimu uliopita tutumie kwa uangalifu kwani kutokana na upungufu wa mvua kunaweza kukawepo kwa changamoto ya chakula" alisema Mahenge.


Aidha Mahenge aliagiza watoto waliochaguliwa kwenda shuleni waende wote na kuwa kumekuwa na changamoto ya uandikishaji wa watoto wa shule za msingi ambao upo chini ambapo wamefikia asilimia 70 tu hivyo ameuomba uongozi wa wilaya hiyo kuongeza bidii ya kuwaandikisha.

Akizungumzia kilimo cha zao la alizeti alisema Mkoa wa Singida ni mkoa pekee hapa nchini ambao wananchi wake hutegemea kilimo cha alizeti na kuwa hawajaanza jana wameanza muda mrefu.

Alisema yapo mazao mengine wanayoyategemea kama ufuta, pamba lakini ukiligusa zao la alizeti lina gusa kila familia na kuwa moja ya kigezo walichokitumia kuomba mbegu Serikalini ilikuwa ni utayari wa wananchi kwenye kilimo hicho.

Alisema jambo kubwa walilolizingatia ni kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora ambazo zinaanzia magunia 15 hadi 20 kwa heka moja na kwa kuliona hilo Rais Samia Suluhu alitoa fedha kwa mkoa wa Singida za kutosheleza tani 465 kwa bei ya 7000 na kuzilipa ambapo aliagiza wananchi walipie Sh.3500 na yeye atachangia hiyo nusu nyingine.

Alisema jambo alilofanya Rais ni kubwa mno kwani hakuna hata benki inayoweza kukupa mkopo huo hivyo wana kila sababu ya kumshukuru.

Dk. Mahenge alisema waliweka utaratibu wa mbegu hizo namna ya kuwakopesha wananchi ambao wanafahamika na wenye uwezo wa kulipa nusu walipe hivyo aliuomba uongozi wa wilaya hiyo kuandaa orodha ya watu ili wajulikane na iwapo itatokea njaa itasaidia kuwabaini waliogoma kukopeshwa.

Mahenge aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kukopa mbegu hizo ambapo wakizipanda na kuvuna watapata fedha za kununulia chakula.

Post a Comment

0 Comments