Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo akielezea taarifa mbalimbali zitakazojadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote,(UCSAF) Justina Mashiba ,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk.Alice Kaijage ,akitoa salamu kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (hayupo pichani),wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Meneja Mkoa wa Dodoma Ferdinand Kabyemela akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (hayupo pichani),mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo akikabidhi zawadi ya kalenda na shajara (Diary) kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo akikabidhi zawadi ya kalenda na shajara (Diary) kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi wakati wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kinachofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) unaofanyika jijini Dodoma.
...........................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameelekeza Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania kushirikishwa na kuwa wajumbe wa kudumu kwenye vikao vinavyosimamia utekelezaji mradi wa kuweka mfumo wa anuani za makazi na postikodi ili ufanyike kwa ufanisi.
Kauli hiyo ameitoa leo Januari 26,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika hilo kwa mwaka 2022/23.
Amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kupeleka maelekezo maalum kwenye Mikoa kwa kuwa viongozi hao ni watu muhimu kushirikishwa ili kufanikisha mradi kukamilika mwezi Mei mwaka huu badala ya miaka mitano ilivyokuwa imepangwa awali.
“Jambo hili ni lenu wengine wafanye kuwasaidieni lakini ninyi ndio muongoze jambo hili, sasa inawezekana mliwekwa pembeni au mlikaa pembeni sasa mwenye sekta anasema twendeni jikoni, Katibu Mkuu simamia warudi jikoni kihalali kwa nyaraka na kwa taratibu wapewe heshima inayostahili,”amesema.
Ameongeza kuwa “Natambua nchi zilizoendelea zimekuwa zikitumia mfumo huu wa anuani za makazi kwa miaka mingi, Tanzania tuliingiza mfumo huu kwenye sera mwaka 2003 na imechukua muda mrefu kuanza kutekelezwa, mkutano wa Umoja wa Posta Duniani ulipitisha kuwepo na anuani za makazi na postkodi, hakukuwa na msukumo wa kutosha sasa viongozi wetu wa kitaifa wametoa fedha kuhakikisha mradi huu unakamilika Mei mwaka huu.”
Pia ameahidi Wizara hiyo itafanya mapitio ya sera na kuboresha kanuni za Shirika hilo ambazo ni za muda mrefu iliziendane na wakati wa sasa wa kidigitali.
Akizungumzia maslahi ya wafanyakazi, Waziri Nape amesema Wizara hiyo itasimamia ipasavyo maslahi yao huku akiwapongeza kwa utendaji wao mzuri uliosaidia shirika kuimarika pale lilipotaka kuyumba.
Amepongeza mapendekezo ya mpango mkakati wa nane wa kibiashara 2022-2026 wenye lengo la kufanya posta ya kidigitali kwa biashara endelevu yanayoendana na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan na matakwa ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Jim Yonazi, amesema umoja wa watumishi wa posta umesaidia kutatua kero mbalimbali na kwasasa Shirika linakua kiuchumi na taswira imezidi kuwa bora.
Awali, Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo, alisema mkutano huo unalenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya taasisi na maslahi ya watumishi.
“Mkutano utakuwa na mambo makuu mawili mafunzo kwa wajumbe wa Baraza kuu lakini pia kikao chenyewe, kwenye mafunzo kutakuwa na mafunzo ya uongozi, ya kumjali mteja, namna ya kupambana na dawa za kulevya, mafunzo ya mifumo, mfumo wa anuani ya makazi ili Mameneja wa Mikoa pamoja na Meneja Mkazi Zanzibar wanashiriki kikamilifu kwenye utekeleza wake,”amesema.
Amesema itajadili utekelezaji wa mpango wa bajeti wa shirika kwa mwaka 2021/22 na mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2022/23 na mapendekezo ya mpango mkakati mpya wa kibiashara wa nane wa shirika ambao ni wa miaka mitano.
0 Comments