Ticker

6/recent/ticker-posts

MAVUNDE AKAGUA UJENZI DARAJA LA MTAA WA NZINJE, AMPONGEZA RAIS SAMIA KUWEZESHA FEDHA TARURA

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akiangalia watalaama wa TARURA wakati ziara hiyo
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akiwa na Diwani wa Kata ya Mkonze, Mh. David Bochela katika ziara hiyo ya ukaguzi.

**************

NA MWANDISHI WETU, DODOMA.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde kwa niaba ya Wananchi wa jimbo hilo, ameishukuru Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassanbkwa kuitengea fedha Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na kuweza kusaidia miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini.

Mh. Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake maalumu akiongozana na Diwani wa Kata ya Mkonze Mh. David Bochela katika ukaguzi wa ujenzi wa daraja kubwa la kivuko katika Mtaa wa Nzinje,Jijini Dodoma.

Akiwa katika eneo la ujenzi, Mh. Mavunde alibainisha kuwa, Daraja hilo ambalo linajengwa chini ya TARURA litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mtaa wa Nzinje na maeneo jirani ambao kipindi cha mvua wamekuwa wakipata mkwamo mkubwa wa kuvuka na kuunganishwa na maeneo mengine kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

"Kwa niaba ya Wananchi wa jimbo Wana Dodoma mjini, tunaishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuitengea fedha TARURA.

Fedha za kutosha kugharamia ujenzi wa barabara, mitaro na madaraja Jijini Dodoma na hali itakayopelekea maeneo mengi kupitika kwa urahisi." Alisema Mh. Mavunde.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19, amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imepokea jumla ya Shilingi Bilioni 330.47 kupitia chanzo cha makusanyo ya mapato ya ndani.

Ambazo ni tozo mbalimbali kwa ajili ya kufungua na kufanya ukarabati wa ujenzi wa miundombinu ya barabara na tayari TARURA imeshasaini mikataba 1687 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 575.37 sawa na asilimia 88 na kazi inaendelea katika Halmashauri zote nchini.

Post a Comment

0 Comments