Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe Nchini Malawi na kupokelewa na Waziri wa Masuala ya Jinsia wa Malawi Patricia Kaliate. Makamu wa Rais yupo nchini Malawi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 11-12 Januari 2022.
Picha - Ofisi ya Makamu wa Rais – Januari 10,2022.
0 Comments