Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (Nguo) na kiwanda cha Viatu vya Idara Maalum ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Januari 8,2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizindua kiwanda cha Nguo cha Idara Maalum ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mtoni KVZ. Januari 8,2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kiwanda cha Nguo na kiwanda cha Viatu vinavyomilikiwa na Idara Maalum za SMZ vilivyopo eneo la Mtoni KVZ. Januari 8,2022 Zanzibar Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipokea maelezo ya namna mitambo mbalimbali ya kutengeneza viatu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa viwanda vya Idara Maalum za SMZ Ramadhan Khamis Ibrahim mara baada ya kuzindua viwanda hivyo . Januari 8,2022 Zanzibar. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishuhudia moja ya kiatu kilichotengenezwa na kiwanda cha viatu cha Idara Maalum za SMZ mara baada ya kuzindua kiwanda hicho tarehe 8 Januari 2022 Zanzibar. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akicheza ngoma ya Mkwaju pamoja na kikundi cha ngoma hiyo mara baada ya kuzindua kiwanda cha nguo na kiwanda cha viatu vinavyomilikiwa na Idara maalum za SMZ tarehe 8 Januari 2022 Zanzibar. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Askari pamoja na wafanyazi wa kiwanda cha viatu na kiwanda cha nguo mara baada ya kuzindua viwanda hivyo eneo la Mtoni KVZ Zanzibar. Januari 8,2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiakbidhiwa zawadi ya kiatu kilichotengenezwa na kiwanda cha viatu kinachomilikiwa na Idara Maalum za SMZ. Januri 8,2022 Zanzibar.
PICHA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
***************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 8 Januari 2021 amezindua Viwanda vya Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) eneo la Mtoni KVZ Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Viwanda vilivyozinduliwa na Makamu wa Rais ni kiwanda cha ushoni na kiwanda cha Viatu. Uzinduzi wa Viwanda hivyo ni shamshamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kuzindua viwanda hivyo, Makamu wa Rais amesema serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ya Mapinduzi ya Zanzibar zimedhamiria, pamoja na mambo mengine, kuimarisha sekta ya viwanda ili kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa na kuongeza ajira.
Amesema Kwa upande wa Tanzania Bara Serikali imedhamiria kujenga uchumi shindani wa viwanda ili kuifikisha nchi kwenye kipato cha kati cha juu huku Dhamira hiyo ikienda sawia na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukuza na kuvutia uwekezaji hususan katika viwanda ili kutimiza ile dhana ya Uchumi wa Buluu.
Makamu wa Rais amewataka Viongozi wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda pamoja na Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo na vya Kati (SMIDA), kutumia Balozi za Tanzania nje ya nchi katika kupata teknolojia rafiki, mitaji na fursa ya kujifunza namna ya kusimamia viwanda hivyo.
Amesema ni muhimu kuwekeza nguvu katika kutafuta masoko kwa kuzingatia mahitaji mahsusi ya wateja wa ndani na masoko ya nje ya nchi kama Comoro na kwingineko.
Aidha Makamu wa Rais Serikali amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika majengo, mashine pamoja na malighafi na kuwataka watumishi wote wa viwanda hivyo kulinda miundombinu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Amesema ni muhimu kwa viwanda hivyo kulinda mazingira mazuri ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kubuni matumizi mbadala ya mabaki ya viwanda (waste).
Akisoma Risala kiongozi wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi Kamishna Rashid Mzee Abdallah amesema kwa kutumia fursa ya kujifunza kwa vitendo kutoka katika viwanda vya Jeshi la Magereza Tanzania , Suma JkT pamoja na Warsha mbalimbali imepelekea kwa muda mfupi viwanda vimeanza kuleta matokeo chanya na kuonesha mwanga wa mafanikio.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed amesema pamoja na kuongeza ajira lakini pia kiwanda hicho kimeondoa changamoto ya muda mrefu iliopata serikali katika kuagiza viatu na sare za Askari kutoka nje ya nchi.
Amesema kuanza kufanya kazi kwa ufanisi kwa viwanda hivyo kunatekeleza adhma ya mapinduzi na serikali kujitegemea.
0 Comments