Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma wakati akiondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma kuelekea Kampala Nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Februari 1,2022.
*************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 1 Februari 2022 ameondoka nchini kuelekea Kampala nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Akiwa nchini Uganda Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kutoa maamuzi ya mwisho ya uwekezaji (Final Investement Decision) katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani nchini Tanzania (EACOP).
Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika katika uwanja wa sherehe wa Kololo uliopo Kampala Uganda na kuhudhuriwa na makampuni mbalimbali ya kimataifa ambayo ni wabia wa mradi huo.
0 Comments