Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO KUMUWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA SADC NCHINI MALAWI



*****************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango hii leo tarehe 10 Januari 2022 anaondoka nchini kuelekea Lilongwe nchini Malawi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 12 Januari 2022.

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa , Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) utakaofanyika tarehe 11 Januari 2022.

Post a Comment

0 Comments