Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA SIASA SINGIDA YARIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI WA MIRADI WILAYA YA SINGIDA NA MANISPAA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba akizungumza wakati akiongoza Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida walipokuwa wakikagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Manispaa. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahende, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Mwang'ima Nyalandu na Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akizungumza kwenye ziara hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace. akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida William Mwang'ima Nyalandu akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Eliya Digha akizungumzia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida..
Mkuu wa Shule ya Ntonge akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili mbele ya kamati hiyo.
Ukaguzi wa madarasa katika Sekondari ya Ntonge ukiendelea.
Wanafunzi wa Sekondari ya Ilongero wakiwa wamekaa katika darasa lililojengwa na fedha zilizotokana na mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19,
Mkuu wa Shule Sekondari ya Ilongero Ramadhani Juma akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa matatu mbele ya kamati hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida Daniel Shani akitoa taarifa ya ujenzi wa Hospitali hiyo
Mhandisi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida, Costantine Stephano akiwa kazini.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Singida ukiendelea.

Mariam Michael akiishukuru Serikali kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya ya Singida ambapo sasa wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kwenda kupata huduma ya afya mjini Singida na maeneo mengine. Michael aliiomba Serikali kuharakisha kuwapelekea vifaa tiba na dawa ili hospitali hiyo ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Singida .
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mandewa, Georgia Maghiya akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa sita mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.
Muonekano wa moja ya darasa kati ya sita yaliyojengwa Shule ya Sekondari Mandewa.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba akizungumza wakati wa ukaguzi wa madarasa sita yaliyojengwa Shule ya Sekondari Mandewa. kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge na Diwani wa Kata ya Mandewa, Baraka Hamisi.
Ukaguzi wa madarasa yule Sekondari Mbandewa ukiendelea iliyopo Manispaa ya Singida ukiendelea. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba na Mkuu wa Shule hiyo, Georgia Maghiya.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua darasa lililojengwa kwa Sh.12.5 Milioni zilizotokana na tozo za miamala ya simu.
Muonekano wa darasa hilo lililojengwa kwa fedha za tozo za miamala ya simu.
Makada wa CCM wakiwa wamesimama mbele ya darasa lililojengwa kwa fedha za tozo za miamala ya simu. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida, Eva Jeremia, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mandewa, Hamisi Shabani Msaghaa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Ramadhani Mtipa.
Wajumbe wa kamati hiyo wakitoka kukagua bweni linalojengwa Shule ya Sekondari ya Mandewa.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi wa barabara mpya ya kilometa 2.6 inayojengwa Kata ya Unyianga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akizungumzia ujenzi wa Zahanati ya Unyianga.
Diwani wa Kata ya Unyianga Geofrey Mdamu akiishukuru Serikali kwa kujenga barabara ya kilometa 2.6 katika kata hiyo.
Ujenzi wa Zahanati ya Unyianga ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Lusia Mwiru akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati ya Unyianga ambapo Mkuu wa Mkoa Dk. Mahenge amechangia Sh. 2 Milioni huku Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akichangia Sh.300,000.
Mjumbe wa Kamati ya siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo (katikati) akicchangia jambo wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua ujenzi wa Zahanati ya Unyianga,
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mitunduruni Anna Igogo akizungumza wakati akiwatambulisha Vijana wa Kikundi cha Chapakazi cha Kata ya Mitunduruni kinachojishughulisha na utengenezaji wa samani.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Said Robert akisoma taarifa mbele ya kamati hiyo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiangalia samani zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Chapakazi ambao wamewezeshwa mkopo wa Sh.10 Milioni na Manispaa ya Singida.

**********************

Na Dotto Mwaibale, Singida.


KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida imekagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Singida Manispaa na kuridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati kamati hiyo ikikagua miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa , Alhaji Juma Kilimba alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo katika halmashauri hizo.

"Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza hasa ujenzi wa madarasa yalitokana kwa fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19," alisema Kilimba.

Kilimba alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwan kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza kutokana na umuhimu wake.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Kilimba alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ambayo kwa mkoa mzima zimetumika Sh.13,444,000,000 kumewaondolea adha ya kusoma katika mazingira yasiyo rafiki kwa wanafunzi kuanzia shule shikizi, msingi na sekondari.

Alisema hivi sasa nchini kote baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kubwa ya kutoa fedha hizo wananchi hawazungumzii tena ujenzi wa madarasa au ukosefu wa madawati kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na kuwa nguvu inaelekezwa kuhimarisha mitaala.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace amewapongeza mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu kwa kutekeleza kwa umakini wa hali ya juu kufanya kazi nzuri ya kusimamia ujenzi wa madarasa hayo kama alivyotaka Rais Samia Suluhu.

"Kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini hakiyake mpeni, Rais Mama Samia Suluhu Hassan hakika ametuheshimisha watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru na kumuombea kwa Mungu" alisema Boniphace.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza wakuu wa shule na viongozi waliosimamia fedha za kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa waaminifu na kufanikisha miradi hiyo.

Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo katika Wilaya ya Singida ni ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari ya Ntonge ambayo yamegharimu Sh.Milioni 40, ujenzi wa madarasa matatu Shule ya Sekondari ya Ilongero ambayo yamegharimu Sh.60 Milioni, ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi Hospitali ya Wilaya ya Singida na nyumba moja ya watumishi ambao umegharimu Sh.340 Milioni 340 na ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Sekondari Mrama ambayo yamegharimu Sh. 40 Milioni.

Katika Manispaa ya Singida miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa madarasa sita katika Shule ya Sekondari Mandewa ambayo yaligharimu Sh.120 Milioni pamoja na samani zake na pia walipokea Sh.12.5 Milioni zilizotokana na tozo za miamala ya simu ambazo zilitumika kujenga chumba kimoja cha darasa.

Miradi mingine iliyotekelezwa katika manispaa hiyo ni ujenzi wa barabara mpya ya Unyianga yenye urefu wa kilometa 2.6 ambayo itakuwa mbadala baada ya barabara ya awali kukatika kutokana na mvua zilizonyesha mwaka 2019 na 2020 ambao ujenzi wake utagharimu Sh.263,117,200.

Mradi mingine ni ujenzi wa Zahanati ya Unyianga na Mradi wa kutengeneza samani wa Kikundi cha Vijana Chapakazi cha Kata ya Mitunduruni ambacho kilikopeshwa Sh.10 Milioni na Manispaa hiyo.

Ziara hiyo iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hizo pamoja na Mkuu wa Wilaya hizo Mhandisi Paskas Muragili.

Leo kamati hiyo itafanya ziara ya namna hiyo katika Halmashauri za Wilaya ya Iramba, Mkalama na Ikungi wakati jana ziara hiyo imefanyika katika wilaya za Manyoni, Itigi, Singida na Singida Manispaa.

Post a Comment

0 Comments