***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Yanga SC imelazimishwa sare ya 2-2 na timu ya KMKM katika mashindano ya Mapinduzi Cup yanayoendelea visiwani Zanzibar.
Yanga imefuzu nusu fainali kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Yanga yaliwekwa kimyani na Heritie Makambo katika kipindi cha pili na bao lingine likifungwa na Feisal Salumu ambaye ndiye nyota wa mchezo huo.
0 Comments