Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI MBAROUK KATIKA MKUTANO WA DHARURA BARAZA LA MAWAZIRI SADC


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameshiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Lilongwe, nchini Malawi. 

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, umetanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji ulioanza tarehe 11 Januari 2021 Lilongwe, Malawi.

Mbali na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali, pia mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha Kamati ya Fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi na kuhudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kutoka nchi wanachama wa SADC.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akishiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Lilongwe, nchini Malawi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC Jijini Lilongwe, nchini Malawi
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ukiendelea Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Mawaziri walioshiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi.

Post a Comment

0 Comments