*********************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kutinga hatua ya fainali mara baada ya kuwaondoa Yanga Sc kwa mikwaju ya penati 8-9 baada ya kumalizika dakika 90 bila kufungana.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ambapo Azam Fc alicheza mpira wa unaovutia licha ya kukosa nafasi nyingi ambazo walizipata.
Mchezaji wa Yanga Yassin Mustafa ndiye aliyekosa penati ambayo alipiga ikaenda juu hivyo mchezaji wa Azam Fc Mudathiri Yahaya akaweza kumalizia mpira wa mwisho na kuwapeleka fainali.
Azam Fc watawasubiri kati ya Namungo fc ama Simba Sc katika Fainali kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
0 Comments