Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA AFYA WA KENYA AWASILI TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA UHURU


***************************

Na.WAMJW-DSM

Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Mhe. Mutai Kagwe awasili nchini kwa ajili ya kusheherekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima.

Mara baada ya kuwasili Mawaziri hao walifanya mazungumzo ya pamoja ambapo Waziri wa Afya Dkt. Gwajima amemshukuru Mhe. Kagwe kwa kufika nchini Tanzania, ikiwa ni ishara ya kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika kuinua Sekta ya Afya.

Naye Mhe. Mutai Kagwe amempongeza Waziri wa Afya Dkt. Gwajima kwa hatua mbalimbali anazochukua katika kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi, hususan katika eneo la mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.

Post a Comment

0 Comments