*******
Watanzania wametakiwa kutembelea vivutio vya ndani lengo likiwa ni kuchochea utalii huo pamoja na kufahamu vivutio hivyo hali itakayosaidia kutunza sehemu zenye mali kale.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa kampuni ya gome safari and adventures Banzi Bryan Msumi wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema utalii wa ndani utasaidia kutunza mazingira pamoja na kufahamu vivutio vinavyopatikana hapa nchini.
Amesema serikali imekuwa ikihamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii hivyo kampuni ya Gome safari and adventures inaunga mkono jitihada hizo kwa kufanya safari za utalii huku mkakati wa mwaka 2022 kampuni hiyo imekusudia kuongeza baadhi ya vifaa vya usafiri ikiwa ni pamoja na magari.
‘’Sisi gome safari and adventure tuna-operate katika mbuga ya saadani, mikumi pamoja na nyerere national park pamoja na vivutio vya mali kale hasa katika maeneo ya majumba ya wakoloni ili wakazi wa Dar es salaam waweze kufika katika maeneo hayo, Amesema Msumi’’.
Aidha Msumi ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluh Hassan katika kuhamasisha utalii huku miongoni mwa changamoto waliyokumbana na mwaka 2020/21 ni janga la corona
Kwa upande wake tour operator wa kampuni ya gome safari and adventures, Salehe Maulid amesema kuwa katika kutekeleza safari za utalii wamekuwa wakizingatia utunzaji wa mazingira huku akitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ya miundominu.
‘’Mazingira yanajumuisha viumbe hai vyote vinavyotuzunguka hivyo ikitokea kundi moja wapo litaharibu basi utalii nchini hautakua na tija kutokana na hali utalii na mazingira yanashahabiana, aliongeza Saleh’’
Hata hivyo Salehe ameongeza kuwa kwa mwaka 2022 kampuni hiyo inatarajia kuja na mpango wautalii wa kijani lengo ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo ya utalii.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa –UN ya mwezi juni mwaka huu imeonesha kuwa watalii wa kimataifa wamepungua takribani bilioni 1 sawa na asilimia 73 mwaka 2020 kutokana na janga la covid-19 huku nchi zinazoendelea zimetajwa kuathirika zaidi kati ya asilimia 60 hadi 80.
0 Comments