Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYA BIASHARA WA MKOA WA IRINGA NA WILAYA ZAKE WANUFAIKA NA ELIMU YA MATUMIZI BORA YA UMEME


Mhandisi Baraka Kanyika kutoka Tanesco Makao Makuu (kulia) akitoa ushauri kwa mteja atumie motor yenye ufanisi (efficiency) nzuri na pia yenye uwezo kulingana na mashine iliyowekwa ili kuokoa gharama za umeme na kufanya kazi vizuri kwa miaka mingi 


Kulia ni Afisa uhusiano kwa wateja mkoa wa Iringa Francis Mbelwa na katikati ni Bi Jennifer Mgendi Afisa masoko makao makuu wakimsililiza mteja wa kiwanda cha kokoto akiwashukuru TANESCO kwa kuwatembelea na kuwapa elimu ya matumizi bora ya umeme. 


Kulia Bi Jennifer Mgendi akichukua changamoto za mteja zinazohusiana na umeme. 


Katikati Bi Jennifer Mgendi kutoka idara ya Masoko Makao Makuu akiongea na mteja kuhusu elimu ya matumizi bora ya umeme na kuchukua changamoto toka kwa mteja zinazohusiana na umeme 

............................................................... 
Timu ya Tanesco makao makuu kitengo cha masoko wakishirikiana na kitengo cha utafiti wameendelea kutoa elimu kwa wateja wa mkoa wa Iringa . 

Zoezi hilo la kutoa elimu kwa wateja wao limefanyika mkoani Iringa pamoja na wilaya zake . 

Elimu hiyo ilihusu matumizi bora ya umeme ili wateja hao wanaotumia umeme waweze kupunguza upotevu wa nishati na kuokoa gharama zisizo za lazima kwa kutumia umeme vizuri. 

Vile vile walipata pia elimu ya usalama wa miundo mbinu kwa kushauriwa watumie mafundi waliosajiliwa kwa usalama wao,na kutumia vifaa vilivyo bora.

Post a Comment

0 Comments