Ticker

6/recent/ticker-posts

WAATALAMU WAKUTANA KUANDAA MKAKATI WA USIMAMIZI RASILIMALI MAJI


Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mhandisi Styden Rwebangira akizungumza katika kikao cha Waatalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii,Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo Mkoani Morogoro Desemba 17, 2021.


Mratibu wa Mradi wa Julius Nyerere kutoka Wizara ya Nishati, Christopher Bitesigirwe akizungumza katika kikao cha Waatalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii,Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo Mkoani Morogoro Desemba 17, 2021.


Waatalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo wakiwa katika kikao cha kundaa mkakati wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde ya Rufiji na Pangani Mkoani Morogoro Desemba 17,2021.

***********************

Hafsa Omar-Morogoro

Waatalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, na taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo Desemba 17, mwaka huu, wamekutana Mkoani Morogoro ili kundaa mkakati wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde ya Rufiji na Pangani ili kuwezesha upatikanaji wa Nishati endelevu ya Umeme nchini.

Katika kikao hicho ambacho wataalamu hao waliwasilisha mada mbalimbali ambazo zitasaidia kuwezesha kuwa na mkakati madhubuti wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde tajwa.

Akizungumza kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mhandisi Styden Rwebangira, alisema kutokana na umuhimu wa vyanzo vya maji kwa ajili ya mito inayotiririsha maji katika mabonde tajwa na kuzingatia wajibu wa Wizara ya Nishati katika ufanisi wa vituo na miradi ya Umeme.

Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine kwa nyakati tofauti walitembelea maeneo ya vyanzo vya maji katika bonde la Rufiji na kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo hayo kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira, uhifadhi wa vyanzo vya maji na matumizi fanisi ya rasilimali maji.

Aidha, Mhandisi Rwebangira, ameyataja maeneo ambayo Wizara imeratibu utoaji wa elimu husika, ni Mkoa wa Mbeya, Njombe, Iringa, Morogoro, Tabora, Singida, Dodoma na Pwani.

“ kutokana na umuhimu wa mabonde haya kwa Taifa, na kwa kuzingatia maelekezo mbalimbali ya viongozi wa kitaifa yaliyotolewa kwa nyakati tofauti, ni wakati muafaka wa waatalamu kutoka sekta mbalimbali kutafakari kwa kina na kwa pamoja na kuishauri Serikali mkakati Madhubuti wa usimamizi wa rasilimali maji katika mabonde hayo”,alisema.

Alibainisha kuwa, Asilimia 36 ya nishati ya umeme unaozalishwa nchini megawati 573 inatokana na chanzo cha maji ambapo vituo vikubwa vya kuzalisha umeme huo pamoja na madakio ya maji yapo ndani ya mabonde ya Pangani na Rufiji.

Ameongeza kuwa, ili kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa bei nafuu, Serikali imeendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia chanzo cha maji kutokana na unafuu wa gharama za uzalishaji ikilinganishwa na vyanzo vingine vilivyopo nchini.

Alisema, Wizara ya Nishati ina jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli zinazowezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika na unaotabirika kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwezesha ustawi wa shughuli za kiuchumi na kijamii nchini.

Alifafanua kuwa, katika jitihada hizo za kuendeleza uzalishaji umeme wa maji, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere wa megawati 2,115 na maandalizi ya kutekelezaji wa miradi ya Ruhudji megawati 358 na mradi wa Rumakali wa megawati 222 yanaendelea.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji Julius Nyerere (JNHPP) kutoka Wizara ya Nishati, Christopher Bitesigirwe, awali akiwakaribsha wataalamu hao alisema, lengo la kikao hicho ni kukaa pamoja la waatalamu hao ili kuweza kuja na mkakati ambao utakuwa wa usimamizi rasilimali maji ya mabonde wa Rufiji na Pangani.

Pia, amewataka watalamu hao kutoa michango yenye tija ambayo itakuwa na manufaa katika Taifa la Tanzania.

Post a Comment

0 Comments