Afisa wa Mamlaka ya Mapato TRA Makame Ame Makame akitoa elimu kwa mlipa kodi Maeneo ya Mwanakwere - Zanzibar.
Afisa Msimamizi wa Kodi Lameck Ndinda akitoa elimu kwa mfanyabiasha kisiwan Unguja maeneo ya Darajani
Afisa Msimamizi wa Kodi TRA Joyce Ng’oja akitoa elimu kwa mlipakodi maeneo ya Darajani.Afisa wa TRA Martenus Mallya na ZRB Zuwena Said wakitoa Elimu ya kodi kwa mfanyabiashara maeneo ya Darajan Unguja.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato TRA Zanzibar akizungumza na Maafisa wa TRA na ZRB katika ufunguzi wa Kampeni ya elimu Kwa mlipakodi Mlango Kwa Mlango Kisiwan Unguja.
****************
Mamalaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) kwa kushirikiana na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wameanza kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango Zanzibar kisiwani Unguja ambayo litafanyika Kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 4/12/2021 hadi 8/12/2021.
Kampeni inalenga kutoa elimu kwa walipakodi ili kuwajengea uelewa wa kutosha juu ya maswala mbalimbali yanayohusu kodi, kusikiliza maoni yao kwa ajili ya kuboresha huduma za kikodi, Kuwakumbusha kulipa kodi stahiki na kwa wakati kuskiliza kero na changamoto walizonazo na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi.
Zoezi hili lilifunguliwa rasmi tarehe 4/12/2021 na Naibu Kamishna wa TRA Zanzibar Juma Bakari Hassan tarehe 4/12/2021 ambapo katika ufunguzi huo aliongelea maswala mbali mbali ikiwemo kutatua changamoto za wafanyabiashara waliotembelewa na kuweza kupata taarifa sahihi Kwa ajili kusajiliwa Kwa wale ambao hawajasajiliwa.
Vilevile aliwahiimiza maofisa wa TRA kutumia lugha nzuri na kuwaelemisha walipakodi kwa ufasaha juu ya wajibu na haki zao , kuzingatia weledi uwajibikaji na uadilifu pia awashukuru viongozi wa ngazi mbali mbali wa Serikali ya Zanzibar Kwa ushirikiano waliotoa katika maandalizi na utekelezaji wa zoezi la Elimu ya kodi mlango kwa mlango.
0 Comments