Ofisa wa TRA Bw.Cosmass Mkinga akitoa maelekezo kwa mmiliki wa lori maeneo ya Mwandege Wilaya ya Mkulanga Afisa wa TRA (kushot) Bw.Joseph Mlimi akitoa maelekezo kwa mmiliki wa lori eneo la Mwandege wilaya ya Mkuranga
Afisa wa TRA (kushoto) Bw.Cosmass Mkinga akikagua lori eneo la mwandege Mkuranga
Afisa wa TRA Bw.Cosmass Mkinga akifanya usajili wa lori kwa mwenye lori eneo la Mwandege wilaya ya Mkuranga
*******************
Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa risiti za EFD katika malori ya mizigo yanayoelekea mikoa ya kusini katika eneo la Mwandege Wilaya ya Mkuranga ambapo zoezi hilo lilianza tarehe 8 /12/2021.
Magari 21 yamekutwa na makosa mpaka kufikia leo tarehe 10/12/2021.
Meneja msaidizi wa Mkoa wa Pwani TRA Bw. Omar Chikwekwe alizungumza kwamba malori hayo yanavizia mida ya usiku kwa kuamini kuwa TRA muda wao wa kazi umeisha pia amewahimiza wafanyabiashara wenye malori, wenye viwanda na wafanyabiashara wanaoiza bidhaa kutokukwepa kutoa risiti kwa manufaa ya Taifa letu.
Zoezi la ukaguzi linaendelea katika njia kuu zote zitokazo Dar es Salaam pamoja na Kariakoo.
0 Comments