Ticker

6/recent/ticker-posts

TECNO WAZINDUA PROMOTION YA KRISMASI RASMI.

Wafanyakazi wa Kampuni za Simu TECNO wakishika Zawadi za Krismasi.
Wafanyakazi wa Kampuni za Simu TECNO wakiwa katika picha ya pamoja jijjni Dar es Salaam.

Zawadi zinazotarajiwa kutolewa katika Promotion ya krismasi.

*********************

Kampuni za simu mkononi TECNO leo imezindua Promotion ya Simu janja kwa ajili ya watumiaji katika kipindi hiki Cha Sikukuu ya Christmas mass na mwaka mpya.

Akizungumzia kuhusu Promotion hiyo Meneja Mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohammed amewaambia watanzania “Msimu huu wa sikukuu chochote unachotaka kuwapa zawadi ndugu, jamaa na marafiki zako msimu huu wa sikukuu, utakipata tecno, unachotakiwa kufanya nunua simu yoyote ya smartphone kutoka TECNO basi na sisi hatutawezi kukuacha hivi hivi”. Pia akaongezea kuwa “mwisho wa mwezi huu ndio kutakuwa na droo ya kushinda zawadi kubwa ya friji, mashine ya kufuria, microwave na zawadi zengine mbalimbali”.

Zawadi izi ya droo zinawalenga wale wateja wote watakao nunua simu za CAMON 18 Series na SPARK 8 Series.

Promotion hii itakuwa nchi nzima katika maduka ya TECNO yenye promotion ambapo zawadi zitatolewa papo hapo dukani kwa wateja watakao nunua simu za POP Series, SPARK Series na CAMON Series.

Ameeleza kuwa ni desturi ya kampuni ya TECNO kuwa na promotion kubwa kipindi iki cha mwisho wa mwaka ambapo ni muda mahususi kabisa wa kutoa shukrani kwa njia ya zawadi kwa marafiki, ndugu, jamaa na wana wamilia yako kiujumla.

Post a Comment

0 Comments