Mkurugezi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH, Dkt, Amos Nungu (wa katikati) Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Kuhusu ushindi wa mbunifu Godfrey Kilimomweshi, kushoto (Fund App) ambaye amekuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya ubunifu, kulia ni Method Rutechura Afisa msimamizi wa mradi wa SAIS.
***********************
TANZANIA imekuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya kimataifa ya kunadi ubunifu katika nchi tano za kusini mwa Afrika zilizoshiriki mashindano hayo nchini Finland mwanzoni mwa Desemba 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu ameyasema hayo leo Desemba 10, 2021 wakati akimtambulisha mshindi wa mashindano hayo Godfrey Kilimwomeshi, ambaye alibuni mfumo wa simu (Mobile App).
Amesema, mfumo huo wa simu unamuwezesha wenye mahitaji ya kupata huduma ya upatikanaji wa mafundi kupitia simu za kiganjani.
"Mwaka huu Tanzania imewakilishwa na wabunifu wawili katika mafunzo ya kukuza ubunifu katika mashindano yaliyoandaliwa na SAIS ambapo jumla ya wabunifu 11 wamepata nafasi ya kunadi bunifu zao mbele ya majaji wa tano, huku Kilimwomeshi akiibuka mshindi ambae pia ni mwanzilishi mwenza na kiongozi wa Fundi App.
Amesema, kwa miaka minne sasa, Tanzania imekuwa ikishiriki katika program ya kuku za ubunifu kusini Mwa Afrika-Southern Afrika Innvoation Support (SAIS) inayofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na nchi tano Tanzania, Botswana, Namibia, Afrika kusini na Zambia.
Amesema kila mwaka, programu hiyo huandaa mafunzo ya kukuza ubunifu kwa wabunifu wa tano nchi zinazoshiriki, mafunzo hayo huambatana na naashindano ambapo mshindi kupata fursa mbali mbali.
Kwa upande wake, Kilimwomeshi amesema zawadi aliyopata ni Euro 3,000sawa na Sh milioni nane na pia alipata nafasi ya kunadai ubunifu wake mbele ya wawekezaji ambapo hadi sasa anafanya mazungumzo na wawekezaji watatu.
Pia, amesema faida nyingine aliweza kukutana na na wabunifu na Kampuni mbali mbali za kimataifa waliyoshiriki katika kongamano la Slush, ambayo ni fursa ya kukutana na wafadhili na wahisani watarajiwa ambao kupitia kwake COSTECH imepanga kuanzisha nao ushirikiano.
Aidha, amewataka vijana kutokukata tamaa katika harakati za kuzitambulisha bunifu zao na pia amewata kupeleka mawazo yao COSTECH ili waweze kuwasaidia kukuza mawazo yao.
0 Comments