Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO),Bw.Mnzava Immanuel,akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Prof.Peter Msoffe wakati akitoa taarifa kuhusu punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo leo Desemba 20,2021 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO),Bw.Mnzava Immanuel,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo leo Desemba 20,2021 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu,akielezea jinsi walivyojipanga kutoa huduma bora kwa wananachi watakaokuja kununua nyama wakati wa punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo leo Desemba 20,2021 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO),Bw.Mnzava Immanuel,akiwaonysha waandishi wa habari Mbuzi pamoja Kondoo waliopo katika Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutoa ya punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo leo Desemba 20,2021 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO),Bw.Mnzava Immanuel,akiwatajia bei ya Mbuzi aliyeshikwa na Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu mara baada ya kutoa ya punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo leo Desemba 20,2021 wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu,akimshika Kondoo anayefungwa katika ranchi hiyo iliyopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 20,2021.
Muonekano wa Mbuzi na Kondoo waliopo katika Ranchi ya Kongwa
......................................................................
Na Alex Sonna, Kongwa
KAMPUNI ya Ranchi za Taifa (NARCO), imetoa punguzo la bei msimu wa sikukuu kwa mbuzi na kondoo ili kuhamasisha wananchi kula nyama hiyo na kupanua wigo wa soko la ndani.
Meneja Masoko wa NARCO, Mnzava Immanuel ametoa kauli hiyo leo Desemba 202,2021 wilayani Kongwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Prof.Peter Msoffe.
Mnzava amesema wamefikia hatua hiyo ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha afya za watanzania ambapo mbuzi 3,000 na kondoo 1,000 aina ya Blackhead Persian(BHP) watauzwa kwa bei ya punguzo la asilimia 33.
Amebainisha kuwa punguzo hilo litakuwa katika Ranchi za Kongwa, Ruvu, Mkata, Kalambo, West Kilimanjaro na Missenyi.
Ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kwamba ulaji wa nyama ya mbuzi na kondoo bado uko chini nchini ikilinganishwa na ulaji wa nyama ya ng’ombe ambao unaongezeka kila Mwaka.
Amehamasisha watanzania kufuga kisasa na kibiashara mbuzi na kondoo ili kukidhi mahitaji ya soko la kigeni na viwanda vya nyama nchini.
Hata hivyo, amesema mahitaji ya nyama ya mbuzi na kondoo katika soko la nje na katika machinjio na viwanda vya nyama vilivyopo na vinavyoendelea kujengwa nchini yanaongezeka na hivyo kutoa fursa ya soko hilo kwa wafugaji.
“Ofa hii ya krismasi na Mwaka mpya itaanza kutolewa kuanzia Desemba 21, mwaka 2021 hadi Januari 10, mwaka 2022 katika ranchi zilizotajwa katika ofa hii,”amesema.
Naye, Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi watakaojitokeza kuchangamkia fursa hiyo.
“Pamoja na ofa hii kila siku katika ranchi yetu tuna chinja ng’ombe kuna nyama nzuri, tunahamasisha wananchi katika kipindi hiki wakaribie waje wapate huduma sahihi kulingana na mahitaji yao,”amesema.
Amesema nyama hiyo ina ubora wa tofauti na mifugo ya kawaida kutokana na kupitia utaratibu wa unenepeshaji.
0 Comments