Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI BYABATO AHUDHURIA MKUTANO WA 40 WA MAWAZIRI WA SADC WA NISHATI NA MAJI NCHINI MALAWI


*************** 

Na Mwandishi wetu - Blantyre, Malawi. 

Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Wakili Stephen Byabato leo tarehe 02 Desemba, 2021 ameshiriki katika Mkutano wa 40 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mkutano huo uliofanyika Blantyre nchini Malawi, umejadili masuala ya Nishati ikijumuisha Umeme, Nishati Jadidifu, Mafuta na Gesi pamoja na masuala ya Maji. 

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri wa Nchi Wanachama 11 zikiwemo Malawi, Afrika Kusini, Zambia, Tanzania, Namibia, Angola, Eswatini, Msumbiji, Botswana, Zimbabwe na Lesotho. 

Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati na Maji tarehe 29 hadi 30 Novemba, 2021 

Naibu Waziri Byabato, aliambatana na baadhi ya Viongozi pamoja na watalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba pamoja na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba.

Post a Comment

0 Comments