Ticker

6/recent/ticker-posts

MTATURU AHIMIZA UMOJA NA MSHIKAMANO ACHANGIA CHEREHANI 10.


....................................................

Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kiislamu( Almadrasatul Tah Dhiibul Islaamiyaa na kuwahimiza viongozi wa dini kuhubiri Umoja na mshikamano.

Aidha,amechangia Cherehani 10 na Seti moja ya Kujifunzia Ufundi Seremala kwa vijana wa chuo hicho.

Akizungumza Disemba 4,katika maadhisho ya chuo hicho kilichopo Kata ya Dung'unyi Wilayani Ikungi,Mtaturu amesema Umoja na mshikamano ukiwepo utachagiza maendeleo.

"Nimefurahishwa na mafunzo mnayofundishwa Vijana hapa, nami kama muwakilishi wenu nawaunga mkono kwa kuwachangia Cherehani 10 na Seti moja ya kujifunzia ufundi Seremala,

Amewaomba wananchi kuliombea Taifa ili kupata mvua na kuondokana na tishio la Ukame.

Mhe Mtaturu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kata ya Dung'unyi kupata Milioni 80 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa katika Shule za Sekondari Dadu na Munkinya.

Post a Comment

0 Comments