Mwenyekiti wa Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mika Likapakapa akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo Kata ya Mang'onyi kwa mwaka 2020/ 2021 kilichoandaliwa na Diwani wa kata hiyo Innocent Makomelo (kushoto) wilayani humo jana. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mang'onyi, Stanley Ipini.
Diwani wa Kata ya Mang'onyi Innocent Makomelo, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2020/ 2021.
Kaimu Afisa Tarafa Ikungi Yahaya Njiku ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo kwenye kikao hicho, akizungumza.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye Diwani wa Kata ya Siuyu Selestine Yunde akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Sepuka, Halima Ng'imba akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Ikungi, Bwanga Akida, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wanawake wa CCM wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Viongozi wa dini wa kata hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea. Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Puma, Joseph Mtaturu na wa pili ni Diwani Viti Maalumu wa kata hiyo, Fatuma Makula.
Kikao kikiendelea.
Wazee wa kata hiyo wakijitambulisha kwenye kikao hicho.
Viongozi wa wachimbaji madini wa kata hiyo wakijitambulisha kwenye kikao hicho.
Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Mang'onyi, Beatrice Gwao akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mang'onyi Lucas Mkwama akisoma Taarifa ya utekelezaji wa miradi.
Yohana Nkuwi alielezea changamoto ya tembo kuvamia makazi ya watu na kutishia usalama wao katika vitongoji vya Mlumbi na Kinyamberu.
Mzee Andrea Andallu akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Singida Robert Malando akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Shule ya Sekondary ya Mang'onyi Shanta, Florence Rwaigamu akichangia jambo.
Muhudumu wa Afya, Lena Claud kutoka wilayani humo akitoa chanjo ya Uviko -19 kwa Mkuu wa Shule ya Sekondary ya Mang'onyi Shanta, Florence Rwaigamu.
Diwani wa Kata ya Mang'onyi Innocent Makomelo (katikati) akiwaelekeza jambo viongozi mbalimbali waliofika kwenye kikao hicho. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye Diwani wa Kata ya Siuyu Selestine Yunde, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Sepuka, Halima Ng'imba, Kaimu Afisa Tarafa Ikungi Yahaya Njiku na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mang'onyi Lucas Mkwama.
Katibu wa Wachimbaji Wadogo wa Wilaya ya Ikungi, Hamisi Nkingi akichangia jambo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sambaru, Saimoni Mwaigaga akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Imamu wa Kijiji cha Tupendane, Juma Kilongo akizungumza kwenye kikao hicho.
Mchungaji Loth Zakaria Sanka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mang'onyi akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mang'onyi Sajenti Philipo Meena, akiwa kwenye kikao hicho.
Muhudu wa Afya, Blaison Shoo akitoa chanjo ya Uviko-19 kwa mkazi wa kata hiyo, Francis Nyasi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kimesema migogoro yote ya ardhi iliyopo wilayani humo itamalizwa ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea kufanya shughuli za maendeleo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa wakati akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo Kata ya Mang'onyi kwa mwaka 2020/ 2021 kilichoandaliwa na Diwani wa kata hiyo Innocent Makomelo wilayani humo jana.
" Migogoro mingi ya ardhi katika wilaya yetu mingi inachangiwa na baadhi ya viongozi wenzetu wa Serikali na si wananchi na inaweza kutatulika na kuwepo kwake inachelewesha shughuli za maendeleo" alisema Likapakapa.
Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi alisema katika wilaya hiyo ipo Kijiji cha Jogolo mpakani mwa wilaya ya Chemba, Manyoni-Itigi na Singida na Uyui Tabora, Iyumbu, Mgungila- Igunga na Singida-Chemba mkoani Dodoma kupitia Kijiji cha Misughaa.
Alisema migogoro yote ya kiwilaya inafanyiwa kazi na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na wataalamu na akaitaja ile ya ndani kwa ndani kuwa upo mgogoro wa Kijiji cha Mponda-Ng'ongosolo, Gulungu, Ulyampiti-Mwau, Mang'onyi-Mlumbi, Sambaru na Chemba.
Alisema migogoro hiyo haina tija kwa kuwa vijiji vingi viliwekewa mipaka kisheria tangu mwaka 1974 na kuwa vijiji zilivyoanzishwa pia viliwekewa mipaka hivyo migogoro ya yanamna hiyo haiwezi kuzuia kuwapelekea wananchi huduma za maendeleo.
Katika hatua nyingine Likapakapa amewaagiza wenyeviti wote wa vijiji wilayani humo kusoma taarifa ya mapato na matumizi ya vijiji vyao ya mwaka 2020/ 2021 na kuwa atakayeshindwa kufanya hivyo hadi ifikapo Januari 10, 2022 ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata mara moja kwani jambo hilo sio la hiari lipo kisheria.
Diwani wa Kata hiyo Innocent Makomelo akizungumzia shughuli za maendeleo zilizotekelezwa katika kipindi hicho kwenye sekta ya elimu alisema jumla ya vyumba 16 vya madarasa na ofisi 7 vimejengwa kwa ajili ya shule za sekondari na msingi.
Alisema vyumba 7 na ofisi 3 vyenye thamani ya sh.140 milioni vimejengwa sekondari ya Mwau na Mang'onyi Shanta na vyumba 9 na ofisi 4 vimejengwa shule ya Msingi Mang'onyi, Taru Mlimani na Mlumbi kwa thamani ya Sh.80 milioni kwa fedha za Serikali.
Alisema vyumba viwili vya Sekondari ya Mang'onyi Shanta vilikarabatiwa na Mgodi wa Shanta na kukabidhi madawati 187 ambapo jumla ya gharama yote ilikuwa ni Sh.Milioni 20.
Makomelo alisema wanaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini Sambaru, mgodi wa Shanta na kampuni ndogo zinazofanya kazi Shanta katika shughuli zote za miradi ndani ya kata hiyo.
Aliwashukuru wananchi wa Kata ya Mang'onyi ambao walitengeneza madawati 130, wananchi wa Tupendane madawati 45 na Sambaru 29 hivyo kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati uliojitokeza mwanzoni mwa mwaka huu.
Alitaja miradi mingine waliyoitekeleza ni ya Afya, Miundombinu ya barabara ambapo Kijiji cha Sambaru kilipata jumla ya Sh.120 Milioni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya maji huku Barabara ya Mang'onyi Ntuntu ikitengewa Sh.330 Milioni na Barabara ya Sambaru-Kipompo-Msule na Misughaa ambayo imetengewa Sh.600 Milioni.
Akizungumzia kuhusu sekta ya kilimo alisema kata hiyo imepokea kiasi cha mbegu za alizeti aina ya Record Tani 1.5 ambapo kila kilo inauzwa Sh.7000 na kuwa kiasi cha mbegu kilichonunuliwa ni kilogramu 172.
Kaimu Afisa Tarafa Ikungi Yahaya Njiku ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo kwenye kikao hicho alisema wilaya hiyo siku zote imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji na ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Akizungumzia changamoto zilizojiri kwenye kikao hicho zinazomuhusu mkuu wa wilaya hiyo kama umeme Shule ya Sekondari ya Shanta na suala la mradi wa maji uliofadhiwa na Uturuki ambao umekwama licha ya wananchi kutumia nguvu zao alisema ataziwasilisha kwa mkuu huyo wa wilaya kwa hatua nyingine ya utekelezaji.
Njiku alitumia nafasi hiyo kumpongeza Diwani wa Kata hiyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo ambapo alisema kata hiyo haikupoteza kura walipomchagua.
Katika kikao hicho ambacho Diwani Makomelo aliruhusu maswali mbalimbali ili kujua changamoto walizonazo wananchi, Yohana Nkuwi alielezea changamoto ya tembo kuvamia makazi ya watu na kutishia usalama wao katika vitongoji vya Mlumbi na Kinyamberu ambapo alijibiwa kuwa tayari taarifa hiyo imepekezwa ofisi husika inayoshughulikia wanyama pori kwa ajili ya kuja kuwaondoa tembo hao na kuwa changamoto kubwa iliyopo ni kuwepo kwa askari wa wanyapori mmoja tu katika eneo hilo kutoka Doloto wilayani Manyoni.
0 Comments