Ticker

6/recent/ticker-posts

MFUMO WA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI KUKAMILIKA MWEZI APRILI 2022


************************

Na Emmanuel Kawau

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema ameitaka ya Kamati ya Maboresho ya Mfumo wa Tiketi za mabasi Kielektroniki kuhakikisha wanayafanyia kazi maoni ya wadau kuhusu tiketi hizo ili ifikapo mwezi wa nne 2022 matumizi ya mfumo huo uzinduliwe rasmi .

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi wakati akisomewa taarifa ya namna mfumo ulipofikia kiutekelezaji amesema tayari wanaendelea kufanyia kazi maoni ya wadau wa usafirishaji ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakaa sawa bila kuathiri yeyote.

"Niseme kuwa kmati hii imehusisha wajumbe kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, LATRA, TRA, NIDC, TABOA na TPSF hivyo naamini haitazidi mwezi wa nne mwakani mfumo wa kukata Tiketi kwa njia za Kielektroniki utakamilika na kuanza kutumika". Alisema Mwita Waitara

Hata hivyo amesema maoni yaliyotolewa na wajumbe na wadau muhimu katika sekta ya usafirishaji TABOA ameyapokea na atayafikisha kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ili yafanyiwe kazi kwa lengo la kuendelea kuboresha mfumo huo wa Tiketi za mabasi kwa njia ya Kielektroniki.

Naibu Waziri Mwita ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa LATRA watahakikisha kuwa maoni yote ya wadau yanachukuliwa na kuchakatwa kwa kushirikiana na wadau wengine hususani maswali ya kikanuni na kisheria.

Amesema mchakato huo utakapokamilika watautangaza rasmi kwa watanzania kupitia vyombo vya habari na maoni ambayo tayari wameshakubaliana na mengine bado na yatahitajika pia kupitishwa na bunge mapema mwakani wataanza nayo Ili kuwe na watoa huduma bora na maelewano mazuri baina yao.

Post a Comment

0 Comments