Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA ZA AFYA KUTOKA NCHI ZA EAC WAKUTANA MJINI ZANZIBAR

Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
 (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

katika ngazi ya Makatibu Wakuu unafanyika leo

tarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini

Zanzibar.


Mkutano huu na mkutano wa ngazi ya Maafisa

Waandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8

Desemba 2021 ni sehemu ya mikutano ya awali

yenge jukukumu la kupitia na kuwasilisha agenda

na mapendekezo ya masuala ya afya ya kikanda

yatakayowasilishwa katika Mkutano wa 21 wa

Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya

ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 10

Desemba 2021.




Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu
 unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mkutano huu unafanyika mjini Zanzibar kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii ndani ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021 Jijini Arusha.

*****************


Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma H. Mrisho (Kulia) akifuatilia Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo tarehe 9 Desemba katika Hotel Verde mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.
Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu, kutoka Kenya, Dkt. Moses Mbaruku (kati) akiongoza mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Chrisophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kenya, Dkt. Kuria Francis.
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Tanzania
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe kutoka Kenya
Ujumbe kutoka Uganda
Ujumbe kutoka Burundi

Post a Comment

0 Comments