************************
Mchezaji mashuhuri wa soka ulimwenguni, Samuel Eto'o ameteuliwa kuwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.
Nyota huyo wa miaka 40, aliyewahi kuichezea timu ya Barcelona kabla ya kustaafu, amesema ni heshima kubwa kwake kuhudumu katika shirikisho hilo ambalo limesababisha apate sifa zote alizonazo hadi sasa.
Eto'o alipata kura 43 kutoka kwa shirikisho la Soka la Cameroon dhidi ya 31 ya mshindani wake wa karibu, Seidou Mbombo Njoya.Eto'o Sasa atalazimika kusimamia mafanikio ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambalo Cameroon itakuwa mwenyeji mwaka ujao.
0 Comments