Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. NCHEMBA: TANZANIA KUENDELEA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akitoa maelezo namna Serikali inavyotoa kipaumbele kwenye masuala ya elimu katika Bajeti zake wakati wa kilele cha mkutano wa WireED, uliojadili namna ya kuboresha elimu duniani kwa kuwekeza rasilimali fedha, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisisitiza jambo wakati akiwasilisha hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuwekeza rasilimali fedha kwenye sekta ya elimu, wakati wa kilele cha mkutano wa WireED, uliojadili namna ya kuboresha elimu duniani, Mjini Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiwa na jopo la viongozi mbalimbali duniani hususan wanaosimamia sekta ya fedha na uchumi wakati wa mjadala wa namna Serikali zinavyopaswa kuwekeza rasilimali fedha katika kuendeleza elimu wakati wa kilele cha mkutano wa WireED uliojadili namna ya kuboresha elimu, Mjini Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ufundi na Elimu ya Juu wa Serikali ya Sierra Leone Dkt. Alpha Tejan Wurie, baada ya kumaliza kuwasilisha mada kwenye kilele cha mkutano wa dunia uliojadili masuala ya uwekezaji wa rasilimali fedha kwenye elimu, ujulikanao kama WirED, uliofanyika Mjini Dubai, Falma ya nchi za Kiarabu.


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Global Partnership foe Education (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakijiandaa kuzungumza kwenye kilele cha mkutano wa RewirEd unaojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Global Partnership foe Education (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd uliojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Global Partnership foe Education (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto)) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakijiandaa kuzungumza kwenye jopo la viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd uliojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakizungumza kwenye kilele cha mkutano wa RewirEd uliojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakisisitiza jambo kwenye kilele cha mkutano wa RewirEd uliojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Dubai)

**************

Na Benny Mwaipaja, Dubai

SERIKALI ya Tanzania imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba itaendelea kuwekeza rasilimali fedha kwa ajili ya kuendelea elimu ili kuwa na jamii iliyoelimika kwa ajili ya kuimarisha rasilimali watu watakaochangia maendeleo ya nchi.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dubai na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwenye kilele cha mkutano unaohusu uwekezaji kwenye sekta ya elimu katika karne ya 21 hasa baada ya janga la ugonjwa wa UVIKO-19 kuzitikisa nchini nyingi duniani.

Dkt. Nchemba amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza Bajeti ya Sekta ya Elimu kila mwaka kadri rasilimali fedha inavyopatikana na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuchangia juhudi hizo za Serikali.

Alisema kipaumbele cha Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anapata elimu bila vikwazo kwa kutoa elimu bila malipo huku akiboresha mazingira ya shule nchini kote.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa nchini Tanzania kuna utashi wa kisiasa wa kuendeleza elimu ambapo bajeti ya elimu imekuwa ikiongezeka kila mwaka na mpaka sasa imefikia zaidi ya asilimia 17 na kwamba huenda siku zijazo ikafikia asilimi 20 ya bajeti yote ya Serikali.

Mkutano wa masuala ya elimu ujulikanao kama WirED umewashirikisha wadau mbalimbali kutoka duniani kote ambapo hoja mbalimbali za kuboresha elimu, ikiwemo kuwawezesha vijana, na kuimarisha masuala ya teknolojia yamejadiliwa kwa kina katika mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments