***********
Na Gift Thadey, Hanang'
BENKI ya CRDB imekanlbidhi mifuko 116 ya saruji nyeupe ya thamani ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya Tumaini ya Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Meneja wa Benki ya CRDB kanda kaskazini, Chiku Issa amekabidhi mifuko hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja kwa ajili ya kuunga mkono wiki ya maendeleo Wilayani Hanang' Iliyofanyika Kuanzia Novemba mosi hadi Novemba 5 ambapo benki hiyo haikupata nafasi ya kushiriki.
Michango hiyo ambayo lengo lake ni kusaidia kukarabati hospitali ya Tumaini ya Wilaya hiyo ilikabidhiwa na meneja huyo Chiku kwa niaba ya mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tanzania, ambapo meneja huyo amesema kuwa michango hiyo imetokana na faida waliyoipata na hivyo wao wamerejesha sehemu ya faida hiyo ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita hasa katika kugusa sekta ya afya katika hospitali ya Tumaini iliyojengwa na Taasisi ya Hope Foundation ya mama Ester Sumaye kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita ambayo sasa inahitaji ukarabati.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja ameishukuru Benk hiyo ya CRDB kwa mchango wao huo na amewaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wake kwa benki hiyo na benki zote zinazoa huduma katika Wilaya ya Hanang' kwa maslahi mapana ya wananchi Wa Hanang'.
Pia Mayanja amezihizimiza kampuni zingine zote kuendelea kutoa sehemu ya faida katika kuboresha huduma za afya na elimu.
Mayanja amewahimiza wananchi wote wa ndani na nje ya Wilaya na wadau mbalimbali ambao hawakuweza kushiriki wiki ya maendeleo na wana nia ya kushiriki kuendelea kuchangia.
Hafla hiyo ya Desemba 7 ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM, wakiwemo wajumbe wa Kamati ya usalama ya Wilaya, DED Hanang' Jennifa Omolo ambaye aliambatana na wakuu wa idara, CHMT, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang' Mathew Darema ambaye aliambatana na kamati ya siasa ya Wilaya pamoja na makatibu wa CCM toka Kata zote na wakuu wa taasisi na wadau mbalimbali.
MWISHO
0 Comments