Ticker

6/recent/ticker-posts

CHAMPION RISE YAANDA TUZO ZA UOGELEAJI


********************

Naibu waziri wa sanaa michezo na utamaduni Paulina Gekule anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tuzo za waogeleaji bora zizoandaliwa na kampuni ya Champion Rise zikilenga kukuza mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Amina Mfaume amesema kuwa tuzo hizo zinafanyika kwa mara ya pili na zitahusisha watu wa rika mbalimbali ikiwemo vijana na watoto na niendelevu.

Aidha amesema washiriki wa shindano hilo ni 60 na tuzo hizo zitafanyika Desemba 19 Jijini Dar es Salaam ambapo viingilio kawaida ni shilingi laki moja VIP milioni moja na corporate table ni milioni moja na nusu.

Kwa upande Meneja Masoko wa kampuni hiyo Ally Nchaaga amewataka watanzania kuachana na dhana ya kuamini kuwa mchezo wa kuogelea ni wa watu wa viwango vya juu bali kila mtu anaweza na anahaki ya kushiriki mchezo huo.

Hatahivyo ametoa wito kwa watanzani kushiriki kwa wingi katika tuzo hizo pamoja na kuchangamkia nafasi hizo kwani tiketi ni chache zilizobaki.

Amewataja wadhami wa tuzo hizo kuwa ni pamoja na kampuni ya Pepsi, Hoteli ya Hyatt Regency, Myrtha Pools na Vision Sports.

Post a Comment

0 Comments