************************
Chama Cha Mapinduzi kimefurahishwa na kupongeza zoezi la ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 97 ya shule za sekondari ndani ya Jimbo la Ilemela kutokana na fedha za mpango wa maendeleo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 kiasi cha shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Tisa na Arobaini zilizotolewa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la wilaya la jumuiya ya wanawake wa chama hicho (UWT) Katibu wa CCM Bi Aziza Isimbula mbali na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa fedha hizo zitakazosaidia kupunguza kero ya michango Kwa Wazazi na changamoto ya watoto kukosa elimu na wengine kuifuata umbali mrefu pia amefafanua kuwa viongozi wa chama hicho Kwa ngazi ya wilaya, kata na matawi wameshiriki katika kusimamia matumizi ya fedha za ujenzi na ubora wa majengo hayo sanjari na kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi huo
'.. Kiukweli tunapongeza na tunaishukuru Serikali, Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya Mkuu wa wilaya yetu Mhe Hassan Masalla, Mbunge na viongozi wenzetu wa ngazi mbalimbali Kwa ushirikiano wa pamoja katika kukamilisha kazi hii ..'
Aidha Katibu Isimbula amewaasa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na kumshukuru Rais Mhe Samia Kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiseke na fedha nyengine kiasi cha bilioni tatu kwaajili ya zoezi la upimaji na upangaji Mji
Kwa upande wake Katibu wa Ofisi ya Mbunge Mhe Dkt Angeline Mabula Kanda ya Kirumba Bi Fatuma Kaloli amefafanua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ameshiriki kikamilifu katika zoezi la ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa hayo kwani amefanya ziara zaidi ya mara mbili kukagua hatua za ujenzi, kutoa ushauri na kuhamasisha wananchi katika kushiriki zoezi la ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa huku akiwaasa viongozi wa maeneo mengine kuiga mfano huo wa viongozi wa wilaya ya Ilemela Kwa namna wanavyoshirikiana katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kupitia kauli mbiu Yao ya 'Ilemela ni yetu tushirikiane kuijenga' na sera ya utatu Kwa maana ya nguvu za wananchi, manispaa na Mbunge
Manispaa ya Ilemela imekuwa ya kwanza katika mkoa wa Mwanza kukamilisha na ukabidhi vyumba vya madarasa kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel kwaajili ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwakani 2022.
0 Comments