Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIARA YA MKUU WA CHUO CHA DAR-ES-SALAM NA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE.


Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Wafanya kazi pamoja na Wanafunzi wa Chuo hicho, katika Ukumbi wa Chuo, huko Chukwani Buyu Wilaya ya Magharibi ‘B’.


Makamu Mkuu Wa Chuo Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Prof.William A.L. Anangisye, akitoa Maelezo na kumkaribisha Mkuu wa Chuo hicho, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Ukumbi wa Chuo huko Chukwani Buyu Wilaya ya Magharibi ‘B’.

Mkurugenzi wa IMS Dkt. Margareth S. Kyewalyanga, akisoma Taarifa ya ajali ya Moto na Mipango iliyowekwa ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Kilichopo Mizingani Wilaya ya Mjini, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chuo hicho Chukwani Buyu Wilaya ya Magharibi ‘B’.


Baadhi ya Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari, wakimsikiliza Mkuu wa Chuo hicho, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Chuo huko Chukwani Buyu Wilaya ya Magharibi ‘B’.

Kamishna wa Kikosi Cha Zimamoto na Ukozi Zanzibar Rashid Mzee Abdallah, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, juu ya hatuwa walizozichukua wakati wa tukio la Moto kutokea katika Chuo hicho ,Kilichopo Mizingani Wilaya ya Mjini.

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiangalia baadhi ya sehemu zilizoungua Moto, za ndani ya Jengo la Chuo hicho, Kilichopo Mizingani Wilaya ya Mjini.

Baadhi ya Sehemu za Ndani zilizounguwa Moto za Jengo la Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salam na Taasisi ya Sayansi za Bahari Kilichopo Mizingani Wilaya ya Mjini.

Picha Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments