Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA YAPIMANA NA MLANDEGE FC VISIWANI ZANZIBAR, YAICHAPA 1-0


****************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga leo imeshuka dimbani kumenyana na Mlandege FC visiwani Zanzibar mechi ya kupimana nguvu mara baada ya ligi kusimama kupisha mechi za Kimataifa.

Yanga imepata ushindi kwenye mchezo huo wa bao 1-0 lililofungwa na Heritie Makambo katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Mashabiki wengi wamejitokeza kushuhudia mtanange huo licha ya mchezo huo kucheza usiku.

Katika mchezo huo Yanga iliwakosa baadhi ya wachezaji wao muhimu ambaoni Shabani Djuma,Feisal Salum, Kibwana Shomari, Dickson Job, Khalid Aucho ambao wapo kwenye majukumu timu ya Taifa.

Yanga itashuka tena dimbani Ijjuma hii kumenyana na KMKM visiwani humo katika mchezo wao mwingine wa Kirafiki na kurudi Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Namungo Fc.

Post a Comment

0 Comments