Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY ATOA SIKU 7 UONGOZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUOMBA FEDHA ZA UJENZI WA SOKO JIPYA KARIAKOO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akiongozana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamadi Masauni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Amosi makalla wakitazama soko la Kariakoo linalohitajika kurekebishwa mara baada ya kuungua hivi karibuni.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ametoa siku saba kwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanaomba fedha zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwaajili ya ujenzi wa soko jipya Kariakoo na ukarabati wa soko la zamani.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo alipotembelea Soko la Kariakoo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa Soko la zamani sambamba na ujenzi soko Jipya la Kariakoo.

Amesema ujenzi wa soko jipya litakuwa na ghorofa 6 kwenda juu na ghorofa 2 kwenda chini hivyo ameelekeza kupewa kipaumbele kwa wafanyabiashara ambao walikuwepo tangu mwanzo katika soko la Kariakoo.

"Nimeona michoro ile ya ujenzi wa soko jipya, sasa tutakuwa tumeongeza idadi ya wafanyabiashara, lile dogo lilikuwa linachukua watu 600 hili jipya litachukua watu kama 2250 kwahiyo nafasi ipo naamini pia uongozi wa mkoa utatenda haki". Amesema

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Masauni amesema katika fedha ambazo wameelekezwa kutoa na Mheshimiwa Rais kiasi cha shilingi Bilioni 32.2, bilioni 6 zitatumika katika ukarabati wa soko la zamani la Kariakoo na zaidi ya Bilioni 26 zitatumika katika ujenzi wa soko jipya.

"Fedha hii ipo tayari na hata kama mkihiitaji leo hii au muda wowote ipo na itatolewa mkihiitaji". Amesema Mhandisi Masauni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Amosi Makalla amesema

Post a Comment

0 Comments