Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, David Concar, katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza, lililofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza lililofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam,
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri wa Uwekezaji Geofrey Mwambe akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Liberata Mulamula akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
...............................................................
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF,) kutumia vyema kikao cha wawekezaji na wafanyabiashara kwa kuwaalika wawekezaji nchini na kuwapokea kisekta na kuwa sehemu ya uwekezeji huo pamoja na kuwahakikishia wawekezaji kutoka Uingereza usalama na mazngira ya uwekezaj nchini.
Waziri Mkuu ametoa wito huo leo wakati akifungua kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC.)
“Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 6.5 kutoka mwaka 2016 hadi 2020 na hivyo, kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika.”
Ameongeza kuwa hivi karibuni Serikali imeendelea kushuhudia uwekezaji mkubwa kutoka kwa makampuni ya Uingereza ikiwemo miradi 956 kutoka Uingereza yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.5 imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania pamoja na mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero (Dola za Marekani milioni 238) na kupatikana kwa leseni ya uchimbaji wa madini ya nickel ya Kabanga.
Waziri Mkuu amemshukuru, Mwakilishi Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza wa masuala ya kibiashara Lord Walney kwa kuitangaza Tanzania kuwa sehemu sahihi kwa ajili ya uwekezaji na biashara hususan kwa makampuni kutoka Uingereza.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw.Andrew Maige amesema utayari wa TPSF wa kushirikiana na wawekezeji kwa ukaribu zaidi na Serikali na kupitia kongamno hilo fursa zaidi zitafunguka kwa watanzania ikiwemo Ajira kwa vijana.
"Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na sekta binafsi na huo ni mwanzo mzuri wa kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya sita katika kujipanua kiuchumi na kujenga uhusiano wa kimataifa". Amesema Bw.Maige
Nae, Mwakilishi Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Walney, amesema Uingereza itaendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo na uwekezaji nchini Tanzania na wataendelea kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kukuza uchumi na uwekezaji.
Kwa Upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara amesema Mkutano huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani unalenga kuongeza kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kutoka Nchini Tanzania kwenda Uingereza ili kuweka usawa katika bidhaa zinazoingia na kuuzwa miongoni mwa Nchi hizo mbili.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe, amesema lengo la kongamano hilo ni kupokea mrejesho wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuhusu mazingira ya ufanyaji wa biashara pamoja na kuboresha maeneo ambayo yana changamoto katika uwekezaji na kwa pamoja kuwa na maadhimio ambayo yatatengeneza fursa za kukuza uchumi na usawa wa kibiashara kwa nchi zote.
Waziri Mwambe amesema, Wizara ya Uwekezaji itaendelea kuendesha makongamano ya uwekezaji na wadau wa Sekta Binafsi pamoja na Nchi washirika katika kuhakikisha wanatengeneza fursa na mazingira bora ya uwekezaji kwa kusikiliza mawazo na changamoto zinazowakabili wawekezaji.
Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, anaeshughulikia Kazi, Uchumi na Uwekezaji Bw. Nurdin Solaga, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuwekeza katika sera ya Uchumi wa Bluu ambapo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetengeneza Mazingira bora ya Kiuwekezaji kwa wawekezaji hususan katika sera ya Uchumi wa Bluu.
0 Comments