Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MAKAMBA ASHIRIKI KONGAMANO LILILOANDALIWA NA TPSF PAMOJA NA PSFU KUJADILI FURSA ZITAKAZOPATIKANA KWENYE MRADI WA BOMBA LA GESI

Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba akizungumza katika kongamano la Mafuta na Gesi lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda kujadili ni namna gani wanaweza kunufaika na mradi wa Bomba la gesi. Kongamano hilo limefanyika leo JJkatika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato akizungumza katika kongamano la Mafuta na Gesi lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda kujadili ni namna gani wanaweza kunufaika na mradi wa Bomba la gesi. Kongamano hilo limefanyika leo JJkatika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Gesi wakifuatilia kongamano la Mafuta na Gesi lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda kujadili ni namna gani wanaweza kunufaika na mradi wa Bomba la gesi. Kongamano hilo limefanyika leo JJkatika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa gesi nchini katika kongamano la Mafuta na Gesi lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda kujadili ni namna gani wanaweza kunufaika na mradi wa Bomba la gesi. Kongamano hilo limefanyika leo JJkatika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na taasisi ya sekta binafsi ya nchini Uganda (PSFU) wameandaa Kongamano la pamoja la Mafuta na gesi ili kujadili Mradi wa Bomba la Gesi kuona ni namna gani wanaweza kunufaika.

Akizungumza katika Kongamano hilo Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba amesema kupitia kongamano hilo litatoa elimu kwa Watanzania na sekta binafsi kwa nchi yetu.

"Mradi huu unauwezo mkubwa hasa kuchangia katika uchumi wa nchi yetu, unauwezo wa kuchangia katika ajira pamoja na kutujengea uwezo kama Watanzania katika sekta hii". Amesema Waziri Makamba.

Amesema katika kila eneo ambalo bomba hilo limepita kuna fursa za ajira mbalimbali kama vile makambi, ulinzi, chakula, usafirishaji, ujenzi na ajira nyingine nyingi.

Aidha amesema Tanzania ina mradi mwingine wa kuchakata gesi mkoani Lindi ambao wameanza mazungumzo kati yao na wawekezaji.

"Kupitia mradi huu, Tanzania na Uganda zinaenda kubadilika kwa kiasi kikubwa kwa maana ya Uchumi wake na masrahi wananchi wa nchi hizo mbili". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Francis Nanai amesema gharama za utengenezaji wa mradi huo zaidi ya dola za Kimarekani 3.5 Bilioni lakini ukiangalia mnyororo mzima wa thamani umezidi dola za Kimarekani Bilioni 20 ambazo zinakaribia tirioni 45.

Amesema wamekutana kufahamu na kueleimishana kuhusu mradi hasa faida zake kwenye suala la ajira.

"Tutaangalia ni namna gani Watanzania wanaweza kunufaika kuhusiana na huu mradi moja kwa moja au kupitia mambo mengine ya kibiashara ". Amesema Bw.Nanai.

Post a Comment

0 Comments