Meya wa Jiji la Zanzibar Mahamoud Mohemed Mussa,akizungumza wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi pamoja na shindano la mchoro wa usalama barabarani kwa shule za msingi zilizopo Zanzibar yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend .
Meneja Mauzo Rejareja wa Puma, Venessy Chilambo,akizungumza wakati wa shindano la mchoro wa usalama barabarani kwa shule za msingi zilizopo Zanzibar yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend .
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Salum Amir Ngayan,akizungumza wakati wa shindano la mchoro wa usalama barabarani kwa shule za msingi zilizopo Zanzibar yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend .
Meya wa Jiji la Zanzibar Mahamoud Mohamed Mussa(wa nne kulia) akiwa na viongozi wengine na wawakilishi kutoka Kampuni ya Puma na Amend wakiangalia mchoro wa shindano la usalama barabarani visiwani Zanzibar ambapo shule tano zimeshiriki
Meya wa Jiji la Zanzibar Mohamoud Mohamed Mussa(watatu kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa Shindano la mchoro wa Usalama Barabarani kwa Shule za Msingi Zanzibar ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Amend Khalid Mohamed Said anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Mtopepo B visiwani Zanzibar.Wengine katika picha hiyo ni viongozi kutoka kampuni ya Puma, Amend na walimu.Utoaji zawadi kwa washindi wa shindano hilo umefanyika Shule ya Msingi Kiembe Samaki
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mtopepo B visiwani Zanzibar Khalid Mohamed Said(aliyevaa kofia) akiwa na wanafunzi wenzake wa shule hiyo wakiwa wameshika kikombe cha ushindi wa mchoro wa Usalama Barabarani kwa mwaka 2021 yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Amend.Utoaji wa zawadi kwa wanafunzi na shule ambazo zimeibuka washindi kwenye shindano limefanyika leo katika Shule ya Msingi Kiembe Samaki ,Zanzibar ambapo Meya wa Zanzibar alikuwa Mahamoud Mohamed Mussa alikuwa mgeni rasmi
Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mtopepo Visiwani Zanzibar Khalid Mohamed Said akiwa ameshika kikombe cha ushindi baada ya kuibuka mshindi wa shindano la mchoro wa usalama Barabarani kwa mwaka 2021.Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Aamend
.........................................................................
Na.Alex Sonna,Zanzibar
WANAFUNZI zaidi ya 40,000 Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kushirikiana na Shirika la Amend kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani visiwani hapa.
Mbali ya kutoa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani, Kampuni hiyo iliandaa shindano la mchoro wa usalama barabarani ambapo shule tano zilizopo Zanzibar zimeshiriki shindano hilo ambapo Shule ya Msingi Mtopepo B imeibuka mshindi wa jumla na kuzawadiwa Sh.milioni nne wakati mwanafunzi wa shule hiyo anayesoma darasa la sita Khalid Mohamed Said akiibuka mshindi wa kwanza na kuzawadia Sh.500,000.
Akizungumza wakati wa tukio la utoaji zawadi kwa shule na wanafunzi walioingia 10 bora katika shindano hilo,Meya wa Jiji la Zanzibar Mahamoud Mohemed Mussa amepongeza uwepo wa mafunzi hayo na kuiomba Puma kuendelea kuyatoa ili wanafunzi wengi zaidi wawe na uelewa wa usalama barabarani.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi Zanzibar kuchukua hatua kali kwa waendesha magari na vyombo vya moto ambao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwani kumekuwepo na wimbi kubwa la ajali ambazo nyingi zinatokana na uzembe wa baadhi ya watumiaji wa vyombo hivyo.
Amesema anaamini malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi hao hasa kupunguza ajali huku akilisisitiza umuhimu wa kuhakikisha Jeshi la Polisi Zanzibar kuchukua hatua kali kwani kumeibuka wimbi la watumia vyombo vya moto amba hawafuati sheria za usalama barabarani na wengta leseni.
"Kuna wimbi la waendesha vyombo vya moto ambao hawana leseni na matokeo wamekuwa wakichangia uwepo wa ajali za barabarani, na kwa mazingira ya aina hiyo utaona haja ya uwepo wa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kupunguza ajali za barabarani.
"Takwimu zinaonesha kumekuwa na idadi kubwa ya watu duniani kote ambao wanapoteza maisha ,hivyo mafunzo hayo ni vema yakaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali,"amesema Meya huyo.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo Rejareja wa Puma, Venessy Chilambo aliyezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Dominic Dhanah, amesema lengo la kutoa mafunzo ya usalama barabarani visiwani Zanzibar ni kupunguza ajali za barabarani hasa ikizingatia kuwa Mji huo idadi ya magari imekua ikiongezeka kwa wingi kila siku.
" Mpango huu wa usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi miaka 9 iliyopita ambapo zaidi ya shule 100 zimefikiwa na wanafunzi zaidi ya 120,000 mikoa mbalimbali wamepata mafunzo hayo kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Tukio hili la utoaji zawadi linahitimisha mradi huu kwa kipindi cha mwaka 2020-2021 uliofanywa na kampuni ya Puma kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la AMEND. Mpango huu ulihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani na uchoraji wa picha katika shule 5, ambapo wanafunzi wasiopungua 20,000 walipata mafunzo hayo," Amesema Chilambo.
Chilambo amesema " Puma tunafanya biashara Zanzibar hivyo hii ni njia mojawapo ya kurudisha tunachokipata kupitia mpango huu. Mafunzo haya ya usalama barabarani na uchoraji kwa watoto wa Shule za msingi ni endelevu na lengo ni kuwaelimisha watoto juu ya usalama barabarani ili wawe mabalozi kwa wengine na kwa wao wenyewe hadi watakapokuwa wamekuwa watu wazima."
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Salum Amir Ngayan mesema kampeni hiyo ambayo ni ya aina yake imekuwa maalum kwa ajili ya kuzuia ajali visiwani Zanzibar kwani kumekuwa na changamoto ya ajali.
Amesema ajali za barabarani zimekuwa zikisababisha vifo vya Watanzania wakiwemo vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa na kwamba ajali nyingi zinatokana na kutoheshimu sheria za usalama barabarani zikiwemo alama."Kuna madereva hawatii alama za barabarani hivyo watoto wakiwa na uelewa wa jinsi ya kuvuka tutakuwa tumepunguzza ajali ambazo si za lazima.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni a Michezo Fatma Hamad Rajab amefurahishwa na utolewaji wa mafunzo hayo kwani yatasaidia wanafunzi kujiepusha na ajali kutokana na mafunzo ambayo wameyapata
Ameongeza hata walimu ambao ndio walezi wa wanfunzi wawapo shuleni watakuwa na kazi rahisi y kuagalia usalama watoto hao wanapovuka barabara.Pia amewapongeza walimu waliosimamia wanafunzi kuchora michoro ya usalama barabarani kupitia shindano hilo kwani mbali ya kushiriki wamesaidia kuibua vipaji vya wachorajo na hilo ni jambo jema.
Kwa upande wake Meneja wa Programu wa Shirika la NVCT ambalo limeshiriki kutoa mafunzo ya usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi Zanzibar Ali Hemed Ali amesema jumla ya shule tano zimepata mafunzo hayo na hadi sasa zaidi ya wanafunzi 40,000 Zanzibar wamefikiwa.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Amend amesema Neema Swai amesema mradi huo mradi ambao umekuwa endelevu na kwa Zanzibar hii ni mara ya pili huku akifafanua kwamba takwimu zinaonesha watu milioni 1.35 wanakufa na wengine zaidi ya milioni 50 wanajeruhiwa na wengi wao ni watoto na watu wenye umri chini ya miaka 25.
"Tunawashukuru NVCT kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa katika kufanikisha utolewaji wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani Zanzibt na tunatambua muhimu wa kuwaanda watu wakiwa wadogo kwani hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa kuheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani.Hivyo tuko Zanzibar kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu hiyo kwa lengo la kupunguza ajali,"amesema.
0 Comments