Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akipitia kabrasha linaloonesha mgawo wa fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO19 kaba ya kutoa maagizo ya utekelezaji wa miradi ya elimu afya na maji kwa Wakuu wa wilaya na Wakurungezi wa Halmashuri zote za Mkoa wa Singida kwenye kikao kilichoketi jana..
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Beatrice Mwinuka akitoa wasilisho kwenye kikao hicho.
Wakuu wa wilaya wakiwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya Wakurugezi wa Hamashauri za Mkoa wa Singida wakisikiliza maelekezo kwenye kikao hicho.
Na Bashiri Salum, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge amewataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya mkoani Singida kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jumla ya vyumba vya madarasa 662 na mabweni mawili kabla ya kufikia katikati ya mwenzi Decemba 2021 ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2022.
Dkt.Mahenge ameyasema hayo jana katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Singida,
Alisema Serikali imetoa fedha za maendeleo kiasi cha Sh.Bilioni 6.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 330 ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2022 na vyumba 332 vya madarasa vitakavyo gharimu jumla ya Sh.Bilioni 6.6 kwa ajili ya ujenzi wa vituo shikizi vya shule za msingi.
Hata hivyo Mahenge amebainisha kwamba katika fedha za maendeleo zilizokuja jumla Sh.160 milioni zitatumika kujenga mabweni mawili katika shule za msingi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Alisema katika kutekeleza mpango wa maendeleo kwa usatwi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19, mkoa umetengewa fedha zaidi ya Sh.Bilioni 27.068 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya afya, elimu na maji.
Hata hivyo Dkt. Mahenge amewataka Wakurugezi wa Halmashauri ya Itigi na Mkalama kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu fedha ambazo zilikuwa bado hazijaingia katika baadhi ya mashule ziweze kuingia na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa.
Dkt. Mahenge amewakumbusha viongozi wote wa hamashauri za wilaya kutosafiri kipindi hiki cha utekelezaji wa miradi hiyo ili kuimarisha usimamizi kama muongozo wa awali ulivyotolewa.
Akimalizia maagizo yake Mahenge amezitaka Halmashuri hizo kufanya manunuzi ya pamoja (bulk procurement) ili kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi hiyo na kuwahimiza Meya, wenyeviti wa halmashuri, watendaji wa halmashauri na madiwani kusimamia miradi hiyo kikamilifu.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akawakumbusha Wakurugenzi hao kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Ofis ya Rais Tamisemi juu ya maandalizi ya utekelezaji wa mpango kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.
Mwaluko akatumia muda huo kuagiza kuundwa kwa timu maalum za mkoa na Halmashauri ambazo zitakuwa zikifuatilia miradi hiyo ya maendeleo ya Afya, Elimu na Maji kama maagizo yalivyotolewa na Wizara ya Tamisemi.
Aidha akawakumbusha kuhakikisha miradi yote inayokamilika pamoja na ununuzi wa vifaa unawekwa alama ya mpango wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO -19 ili kuzitambua na kuweza kutofautisha.
Tovuti za Halmashauri pamoja na Mkoa zitumike kikamilifu kutangaza kazi za utoaji wa huduma kwa wanunuzi wa vifaa na mafundi ili atakayeweza kutoa huduma stahiki apate fursa hiyo, alikaririwa Dorothy Mwaluko.
Awali katika wasilisho lake Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Beatrice Mwinuka akabainisha kwamba katika jumla ya fedha zote zilizokuja wametanga Sh.Bilioni 13.4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu msingi ambayo ndiyo itakayotumika katika ujenzi wa vyumba 632 na mabweni mawili.
Aidha akaendelea kufafanua kwamba jumla ya Sh.Bilioni 9.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na ufuatiliaji wa Afya ya msingi ambapo kutakuwa na ujenzi na ununuzi wa vifaa vya huduma ya dharura (EMD), ujenzi wa majengo ya wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na unuuzi wa X-rays.
Beatrice akaendelea kueleza kwamba fedha hizo zimetengwa kwa ajilia ya uboreshaji wa miradi tisa ya maji itakayogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 4.04 katika wilaya ya Iramba , Mkalama, Singida Ikungi, Manispaa ya Singida pamoja na wilaya ya Manyoni.
0 Comments