Ticker

6/recent/ticker-posts

VODACOM YAPANUA HUDUMA KIDIGITALI, YASHIRIKIANA NA KAMPUNI 10 ZA BIMA KUPITIA M-PESA




*****************************

KAMPUNI Ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Vodacom M- Pesa imetangaza ushirikiano mpya na mashirika ya makubwaa kumi ya bima nchini kupitia mfumo wao wa VodaBima ili kushirikiana na Serikali katika lengo la kukuza upatikanaji wa bima kutoka kiwango cha asilimia 0.6 ya pato la Taifa (GDP,) na kufikia walau asilimia 5 ifikapo 2030.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa Epimack Mbeteni amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma kwake mwaka huu, VodaBima imekuwa chachu ya upokeaji wa huduma za bima nchini kwa kutoa huduma hiyo kidigitali kwa watumiaji zaidi ya 50,000.


Amesema, wana mategemeo makubwa ya kiuchumi kwa taifa na jamii kwa ujumla kupitia ushirikiano huo uliohusisha kampuni za bima za Britam Insurance, Alliance Insurance, Jubilee Insurance, Zanzibar Insurance Corporation (ZIC,) Bumaco Insurance, National Insurance Corporation (NIC,) UAP Insurance, Sanlam Insurance, Heritage Insurance na Mayfair Insurance.


" Lengo kuu la Vodacom ilikuwa ni kurahisha huduma za bima kwa watanzania kupitia simu za mkononi. Tumeweza kupunguza gharama za upatikanaji kwa bima na kurahisha mchakato mzima wa kuuweka kwenye mfumo wa M-Pesa na leo tunawapatia VodaBima iliyoboreshwa ambayo ni kubwa na yenye huduma nyingi....kwa kushirikiana na makampuni mengi zaidi ya bima kwenye mfumo wa VodaBima tutegemee mapinduzi makubwa ya teknolojia na Maendeleo ya kiuchumi." Amesema Mbeteni.


Aidha amesema, Serikali imeanzisha mfumo wa kutoa stika za kidigitali na kupitia VodaBima wateja watapata fursa ya kulipa kidogo kidogo kupitia akaunti zao za VodaBima mwaka mzima na kupatiwa ujumbe pale ambapo bima zao zinapokaribia kuisha muda wake.


"Tunawashukuru washirika wetu wapya na tunategemea kuwa huduma hii mpya itaongeza matumizi ya bima nchini.....na kwakuwa bima kubwa inapatikana kwenye VodaBima nantuna watoa huduma wengi zaidi watumiaji wanaweza kununua bima zao na kufuatilia malipo kutoka popote nchini bila kufika katika ofisi za mawakala. Hii ni hatua moja zaidi katika safari yetu ya kuleta mabadiliko ya kidigitali nchini." Amesema.


Akizungumza kwa niaba ya makampuni 10 ya bima Mwenyekiti wa Chama cha Watoa huduma ya Bima Tanzania Hamis Suleiman amesema Vodacom Tanzania wamekuwa wabunifu katika kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini.


"Tunachokiona leo ni matokeo ya ushirikiano unaolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za bima kwa watanzania, tunatumia mtandao mpana wa Vodacom kutimiza mahitaji ya soko na ninaamini kuwa ushirikiano huu utatuleta karibu zaidi na malengo yetu ya bima nchini." Ameeleza Suleiman.


Kwa upande wake kamishina wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma amesema dhamira yao ni kujenga, kutetea na kuendeleza soko jumuishi lenye tija na salama kwa watumiaji wa bima.


"Tunafurahi kuona wadau wa mashirika binafsi wakileta ubunifu kwa utoaji wa huduma za bima kwa Taifa, Vodacom ni mfano wa kuigwa na litaongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa matumizi ya huduma za bima nchini." Amesema.


Awali akizungumza katika hafla hiyo Meneja masoko was huduma za kfedha kutoka Vodacom Noel Mazoya amesema kampuni hiyo imejizatiti kupeleka taifa katika matumizi ya fedha kidigitali.


Amesema walianza na shirika la Bima la Britam na sasa wana washirika 10 watakaojenga ushirikiano mkubwa utakaoioeleka Tanzania mbele katika kukuza uchumi na sekta ya bima kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments