Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akipokea hati ya maalumu kutoka kwa Bi. Preeti Sinha Katibu Mtendaji wa UNCDF. Hati hiyo ni uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano na utoaji fedha kwa Tanzania katika kuimarisha miradi ya kimkakati ya kuchochea maendeleo. Maeneo yatakayonufaika ni pamoja na sekta ya Maji, Mazingira, Afya na Mipango miji. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikabidhi hati ya uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano na utoaji fedha kwa Tanzania iliyotolewa na UNCDF kwa sehemu ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Glasgow. Kutoka kushoto ni Dkt. Emma Liwenga Msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt Andrew Komba Mkurugenzi wa Mazingira, Bi. Farhat Mbarouk, Mkurugenzi wa Mazingira - Zanzibar na Bi. Catherine Bamwenzaki Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais.
Dkt. Andrew Komba akiteta na Bi. Preeti Sinha Katibu Mtendaji wa UNCDF mara baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi hati ya uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano na utoaji fedha kwa Tanzania katika kuimarisha miradi ya kimkakati ya kuchochea maendeleo. Maeneo yatakayonufaika ni pamoja na sekta ya Maji, Mazingira, Afya na Mipango miji.
0 Comments