Ticker

6/recent/ticker-posts

TOENI HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO MUWAFIKIE WENGI-DKT.JINGU


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kilichopo Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.Kamishina wa Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt.Nandera Mhando akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Judith Kimaro akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu (katikati) akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia ambao umefanyika leo Jijjini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wakishiriki katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia uliofanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii,(ISW) leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo yya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.John Jingu (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa KOICA Tanzania Bw.Kyucheol Eo akizindua Kituo cha Elimu,Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia hafla ambayo imefanyika katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii leo Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amewaasa watumishi wa Kituo cha Elimu, ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kuanza kutoa huduma kwa njia ya mtandao ili kuweza kufikia watu wengi zaidi na kupunguza msongamano pindi wateja wakatapo kuwa wengi.

Ameyasema hayo leo wakati akizindua Kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kilichopo chini ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii jJijini Dar es Salaam na kuhududhuriwa na wadau mbalimbali wa taasisi hiyo.

Dkt. Jingu ameeleza jinsi kituo hicho kilivyo na uhitaji mkubwa katika jamii yetu kwani kuna matatizo mengi katika jamii yetu ikiwemo mafarakano ya ndoa, kifamilia, misongo ya mawazo kutokana na ukosefu wa vipato toshelezi, na ajira, kukata tamaa kutoka na magonjwa sugu,watoto wa mitaani, uraibu wa dawa za kulevya, masuala ya VVU na Ukimwi na matatizo mengi ambayo yanaikumba jamii yetu ya Watanzania.

"Ninaipongeza Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa siku zote kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wadau kutoa huduma za ushauri na msaada wa kisaikolojia pindi majanga yanapojitokeza mfano maafa ya Moto mjini Morogoro ambapo Taasisi ilikwenda kutoa msaada kwa wahanga wa ajali hiyo ya moto". Amesema Dkt.Jingu

Dkt. Jingu ameuasa uongozi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kukitunza na kukiendeleza kituo cha hicho cha elimu, Ushauri na Msaada wa kisaikolojia ili kiendelee kuwa msaada kwa Jamii yetu.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amesema kukamilika kwa kazi ya kukarabati kituo hicho kutaboresha mazingira ya utoaji huduma lakini pia kutarahishisha upatikanaji wa huduma.

"Kituo hiki kimejielekeza kupanua utoaji wa huduma na kinakwenda kutoa huduma katika maeneo mbalimbali kama Ushauri wa mahusiano ya ndoa, Ushauri wa malezi na makuzi ya watoto na vijana,Ushauri juu ya uratibu na marekebisho ya tabia,Elimu na ushauri kuhusu sheria za kazi, Elimu na ushauri kuhusu migogoro ya kazi, Ushauri wa kifamilia, Ushauri wa kisaikolojia na Elimu ya Afya ya uzazi kwa vijana". Amesema Dkt.Joyce.

Amesema Taasisi ilianza kutoa huduma za ushauri mwaka 2007 kupitia kituo wakati huo kikijulikana kama Counselling and Information Center. Kituo kilitoa huduma kwa jamii inayotuzunguka, kwa wafanyakazi na wanafunzi wa Taasisi hasa katika masuala ya upimaji wa VVU na ushauri nasaha, uraibu wa madawa ya kulevya, masuala ya kisaikolojia na magonjwa yasioambukiza.

Post a Comment

0 Comments